Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati
akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema),
Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako
tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo
majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya
Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na
wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema:
“Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge
litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge
la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema
sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema
Wassira. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Wassira alisema wajumbe wa Bunge la Katiba
walitunga Kanuni za Bunge hilo na miongoni mwa waliokuwa walimu wa
kanuni hizo alikuwa Ismail Jussa na Tundu Lissu ambao ni wajumbe wa
Ukawa.
“Kanuni tuliyotunga ambayo haipingani na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ni Bunge hilo kuwa na mamlaka ya kubadili,
kurekebisha, kuboresha na kadhalika,” alisema Wassira na kuongeza: “Sasa leo wenzetu baada ya kuamua kutoka wanasema
tunavunja sheria eti kwa sababu tunapingana na mawazo ya wananchi. Hiyo
siyo sawa. Tunapingana na maoni yapi ya wananchi?
Wassira alisema kama ni hoja ya maoni ya wananchi,
upande wa Zanzibar asilimia 60 walitaka Serikali ya mkataba lakini
rasimu iliyopo mbele ya Bunge Maalumu la Katiba haina mapendekezo ya
mkataba.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema aliwasihi wajumbe wa Ukawa warejee bungeni, akisisitiza kuwa
Katiba Mpya itapatikana kwa maridhiano na si kwa wajumbe kuasi Bunge. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mabilioni Bunge la Katiba utata
Wabunge wa upinzani wamehoji kiasi cha fedha
kilichotumika kugharimia awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu la Katiba.
Kuhoji huko kumetokea wakati, Wizara ya Katiba na Sheria ikisema Sh21
bilioni zimetengwa kwa ajili ya awamu ya pili ya Bunge la Katiba
linalotarajia kuanza vikao vyake Agosti 5, mwaka huu mjini Dodoma.
Naibu Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa wizara hiyo,
Rashid Ali Abdalla, akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu Makadirio
ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2014/15 alisema zipo ndimi mbili kutoka
kwa mawaziri watatu ambazo zinasababisha mkanganyiko wa kiasi
kilichotumika katika Bunge hilo, jambo linalohitaji kuhojiwa na kupata
ukweli.
Abdalla alisema kwa nyakati tofauti, Waziri wa
Fedha, Saada Mkuya amekaririwa akisema Bunge hilo lilitumia Sh27 bilioni
kauli iliyoungwa mkono na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge) William Lukuvi. Hata hivyo, alisema utata ulijitokeza baada ya
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kueleza kuwa Bunge la
Katiba lilitumia kiasi cha Sh24.4 bilioni kiasi ambacho kinatofautiana
na wenzake.
Mwandosya ataka wimbo mpya
Katika hatua nyingine; Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Profesa Mark Mwandosya ametoa hoja ya kuubadilisha Wimbo wa Taifa
ili kulinda uzalendo Tanzania. Alitoa hoja hiyo alipokuwa akichangia Bajeti ya
Wizara ya Katiba na Sheria kwa kueleza kuwa, wimbo unaotumika sasa ni wa
kuazima kutoka Afrika Kusini, hivyo ni kama kuenzi utamaduni wa huko
badala ya kudumisha na kujenga uzalendo kwa Watanzania, hasa vijana.
“Tufikirie kuwa na wimbo wenye hadhi ya Kitanzania
ili kuendeleza uzalendo zaidi na kuachana na huu uliopo. Tunaweza hata
tukautumia wimbo wa ‘Tanzania… Tanzania’ ambao ni wa kwetu tofauti na
uliopo ambao tumeuazima,” alisema Profesa Mwandosya.
Chanzo: Mwananchi
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: Mwananchi
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment