Madai ya wajumbe kutaka waongezewe
posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya
wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo
iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.
Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu
Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo
wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Wednesday, February 26, 2014
DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI...!!!
Askari akimwongoza mtuhumiwa Mustafa Kitano, anayedaiwa kutoa huduma za utabibu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinyume na utaratibu,Picha na Michael Jamson
Dar es Salaam. Maofisa Usalama wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamemkamata mtu anayedaiwa kutoa huduma kwa wagonjwa kinyume cha utaratiba na kwamba, amekuwa akiwatapeli wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminieli Eligaesha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mustafa Kitano na kwamba, amekuwa akitumia majina ya Dk Nyirabu na Koba, alikamatwa wakati akimsaidia mgonjwa mmoja.
Eligeisha alisema Februari 22 mwaka huu walipata taarifa kutoka kwa Hussein Haji kuwa, kuna daktari anaitwa Koba alitaka kumtapeli Sh200,000 ili amtafutie kazi ya udereva kwenye tawi la MNH lililopo Kahama Shinyanga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
OPERESHENI DHIDI YA WAASI WA UGANDA ADF
Waasi wa Uganda ADF.
Operesheni zinaendelea katika wilaya
ya Beni, jeshi la serikali limetangaza kuwa, operesheni hizo,
zimelipelekea jeshi hilo kuyakomboa maeneo kadhaa, toka mikononi mwa
waasi.
Operesheni dhidi ya waasi wa Uganda ADF wanaojihifadhi katika misitu
ya wilaya ya Beni mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiwa zinaendelea,huku wanajeshi wakiwa wamepelekwa katika eneo hilo, raia wa mji na wilaya za Beni wameanza kulalamikia usalama wao,kutokana na jinsi wanavyo nyanyaswa na wanajeshi wa serikali. Ili kukomesha vitendo vya unyanyasi wa raia, jeshi la Congo limelivalia njuga suala hilo.
Mwandishi wetu John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Beni. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
ya wilaya ya Beni mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiwa zinaendelea,huku wanajeshi wakiwa wamepelekwa katika eneo hilo, raia wa mji na wilaya za Beni wameanza kulalamikia usalama wao,kutokana na jinsi wanavyo nyanyaswa na wanajeshi wa serikali. Ili kukomesha vitendo vya unyanyasi wa raia, jeshi la Congo limelivalia njuga suala hilo.
Mwandishi wetu John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Beni. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo, dw.de.com/swahili.
Tuesday, February 25, 2014
'ANAYEONA POSHO HAITOSHI AFUNGASHE VIRAGO'
Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
NYALANDU APANGUA WAKURUGENZI MALIASILI
Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaondoa katika nyadhifa zao, Wakurugenzi mbalimbali kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Hatua ya Nyalandu imekuja ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Bunge la Desemba 22, 2013 lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Nyalandu alisema: "Namwondoa Prof Alexander Songorwa (Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori) na kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo."
Alisema pia kuwa amemwondoa Mkurugenzi
Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho
kwenye nafasi hiyo na Dk Charles Mulokozi ameteuliwa kushika wadhifa
huo.
Mwingine aliyeteuliwa ni Julius Kibebe
kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili, nafasi iliyoachwa wazi na
Sarakikya wakati Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu,
Nebbo Mwina anabaki kwenye nafasi yake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
KUANGALIA MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA BURE
Washabiki wa mpira wa miguu nchini
watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake
(Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya
kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa
(Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga Stars ambayo ilipoteza mechi ya
kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 iko
kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma
ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi
(Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba,
Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga kutoka
Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa (Februari
26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye
atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo: TFF
MILIPUKO YA MABOMU YARINDIMA Z'BAR
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar. Watu wanne wamejeruhiwa
baada ya milipuko minne inayoaminika kuwa ni mabomu kutokea katika
maeneo matatu tofauti Zanzibar.
Katika moja ya matukio hayo, watu
wanne walijeruhiwa, mmoja akikatika mguu, katika eneo la Unguja Ukuu,
Mkoa wa Kaskazini Unguja. Majeruhi wawili wamelazwa katika Hospitali ya
Mnazi Mmoja, Unguja.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Mkoa wa
Kusini Unguja, Hamad Said Masoud alisema mlipuko wa kwanza ulitokea juzi
katika eneo la Fuaoni Maili Nne wakati watu wasiojulikana waliporusha
kitu kinachoaminika kuwa ni bomu wakati waumini wa Kanisa la Evangelist
wakiendelea na ibada ya Jumapili.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan
Omar Makame alisema tukio la juzi, kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu
kilirushwa wakati waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada na kutoa
mlipuko na kishindo kikubwa. Alisema wakati wakiendelea na uchunguzi wa
tukio hilo, milipuko mingine mitatu ilitokea jana.
Katika mlipuko wa kwanza kwa jana
uliotokea saa 6.30 mchana katika kituo kimoja cha fundi vyuma
aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah huko Unguja Ukuu ndiko
kulikokuwa na watu waliojeruhiwa.
Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Pandu Haji Pandu aliyekatika mguu na Shaaban Khamis Ibrahim ambaye aliumia sehemu za kiuno.
Hamad alisema mtu mmoja aliokota chuma kizito na kukipeleka kwa fundi akitaka atengenezewe nanga kwa ajili ya uvuvi.
Alisema mhunzi huyo alipokea kazi hiyo
na alipokuwa akijiandaa kwa matengenezo ndipo mlipuko huo ulipotokea.
Mlipuko huo ulitokea sambamba na mwingine katika Mgahawa wa Mercury's
uliopo Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi na kusababisha huduma za chakula
kusitishwa kwa muda.
Tukio la mwisho lilikuwa saa 7:15
mchana katika Kanisa la Anglikana, Mkunazini. Katibu wa Kanisa hilo
Dayosisi ya Zanzibar, Nuhu Saranya alisema: "Nilisikia kishindo cha
mlipuko, wakati nikitafakari ni kitu gani hicho, nikasikia mlipuko wa
pili nje ya kanisa letu," alisema.
Mmoja wa majeruhi, Mohamed Ibrahim
alisema hakujua kilichotokea huku akilalamika kuwa masikio yake
hayasikii vizuri kutokana na kishindo hicho.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Monday, February 24, 2014
FANYA HAYA KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU...!!!
Sio
mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi
katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya
kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano
yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe
majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako,
hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha
yako ya mapenzi. Makala hii inaeleza
mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu,
jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.
1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa
nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza
unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha
kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza
kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala
mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili
kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Wednesday, February 19, 2014
UGANDA WATUNGA SHERIA KALI KWA WANAOVAA 'MINI SKIRT'
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,
ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na
hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha
zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi
sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha
kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kampala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
BOKO HARAM BADO NI HATARI NIGERIA
Taarifa kutoka nchini Nigeria,
zinasema kuwa kumekuwa na mashambulizi mabaya sana dhidi ya wakazi wa
mji wa mpakani wa Bama, siku moja baada ya msemaji wa Rais kusema kuwa
jeshi linashinda vita dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram.
Seneta wa jimbo la Borno, Ahmed Zanna ameambia BBC kuwa mashambulizi hayo yaliyotokea Jumatano asubuhi yalidumu kwa masaa 5
Siku ya Jumanne, msemaji wa jeshi Doyin Okupe, alisema kuwa jeshi limeweza kudhibiti hali.
Zaidi ya watu 254 wameuawa mwaka huu pekee na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Maelfu wameuawa tangu Boko Haram kuanza vita dhidi ya serikali mwaka 2009.
Taarifa ya bwana Okupe, ilitofautiana na matamshi ya gavana wa jimbo la Borno ambalo ni kitovu cha Boko Haram.
Gavana Kashim Shettima, ametoa wito wa kutaka
wanajeshi zaidi na ambao wamejihami vilivyo kupelekwa katika jimbo hilo,
kuliko vikosi vya usalama vilivyoko katika jimbo hilo.
Taarifa kuhusu mashambulizi ya leo bado
hazitajitokeza lakini wakazi wa eneo hilo wamewasiliana na idhaa ya BBC
Hausa kuhusu mashambulizi ya leo. Mji huo hata hivyo umewahi kushambuliwa katika siku za nyuma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo BBC
TAHADHARI YA MVUA KUBWA FEB 19-21/2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 18 Februari, 2014
TAARIFA KWA UMMA: VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA.
Taarifa Na. 201402-03
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 8:30 Mchana
Daraja la Taarifa:- Tahadhari
Kuanzia: Tarehe 19 Februari, 2014
Mpaka: Tarehe 21 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa ni vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kwa siku.
Kiwango cha uhakika:- Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni Kanda
ya kati (mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini magharibi
(mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe) na maeneo ya kusini (Mikoa ya Ruvuma na Morogoro).
Maelezo:-
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo
wa hewa katika rasi ya Msumbiji. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta
upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:-
Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo
hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada:-
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Monica Mutoni
Public Relation Office
Tanzania Meteorological Agency
VITA VYAZUKA TENA MALAKAL, SUDAN KUSINI
Mapigano yanaripotiwa kuzuka
Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu serikali na waasi kutia saini
makubaliano ya kusitisha vita mwezi Januari.
Waasi wanaomtii makamu wa Rais wa zamani Riek
Machar, wameshambulia mji wa Malakal, ambao ni mji mkuu wa jimbo la
Upper Nile linalozalisha mafuta kwa wingi.Majeshi ya serikali, yamepambana vikali na waasi hao katika maeneo tofauti ya mji huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Juba, (Toby Lanzer), amezitaka pande zote kwenye mzozo huo, kulinda raia.
Makabiliano hayo bila shaka yanazua wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika visima vya mafuta Kaskazini mwa nchi. Mafuta ya Sudan Kusini ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo BBC Swahili
CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE...!!!
Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta
kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya
upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala
hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati
wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo
cha kuvuruga amani ndani ya nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
"Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo
na kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa
Chadema kuvuruga amani nchini," alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni
moto.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa
Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta
alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo
watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya
malalamiko yao.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri
Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya
wapinzani badala ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia
vyombo husika ambavyo ni polisi na majeshi na mahakama. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo:Mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)