WAWAKILISHI wa
Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga leo
inatarajiwa kushuka dimbani ikiwa ughaibuni kwa kuumana na Komorozine ya
Comoro katika pambano la marudiano la michuano hiyo.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye
uwanja wa Sheikh Said Mohamed International uliopo mji wa Mitsamihuli na
Yanga ina kazi nyepesi ya kukamilisha ushindi mnono iliyopata katika
mechi yao ya nyumbani ilipoisasambua Komorozine mabao 7-0.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Comoro
zilizoripotiwa na mtandao wa klabu hiyo ni kwamba mara baada ya juzi
jioni kufanya mazoezi mepesi katika uwanja mdogo wa hotel ya Retaj,
Yanga ilijifua tena jana asubuhi majira ya saa 5 ausbuhi katika Uwanja
wa Sheikh Said kwa ajili ya kuuzoea tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der
Pluijm amesema anashukuru kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo
na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja hivyo anapata fursa ya kuchagua
amtumie nani katika mchezo huo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz