Saturday, December 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 28, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

LUMBESA LA VIPODOZI FEKI LAKAMATWA IRINGA


 Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana. (Picha na Denis Mlowe)

Friday, December 27, 2013

MAGAZETI LEO IJUMAA DESEMBA 27, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

HII HAPA NDIO SIRI YA PINDA KUNUSURIKA

*Katibu Umoja wa Wanawake aadhirika kikaoni
*Wabunge 178 waomba kikao na Kinana

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Ijumaa iliyopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliponea chupuchupu kung’olewa uenyekiti wa kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kikao hicho (party caucus) kilifanyika baada ya hali ya hewa bungeni kuchafuka baada ya kuwekwa hadharani bungeni ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyosomwa na Mwenyekiti wake James Lembeli.

Ripoti hiyo ilihusu tathmini ya upungufu kadha wa kadha uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, upungufu ulioibua mjadala mzito bungeni, na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.

Mawaziri hao ni Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na David David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Hata hivyo habari zilizopatikana zilisema mawaziri hao waling’olewa kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete.

Thursday, December 26, 2013

RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO ALHAMISI

15:45 Hull City Vs Manchester United
18:00 Aston Villa Vs Crystal Palace
18:00 Cardiff City Vs Southampton
18:00 Chelsea Vs Swansea City
18:00 Everton Vs Sunderland
18:00 Newcastle United Vs Stoke City
18:00 Norwich City Vs Fulham
18:00 Tottenham Hotspur Vs West Bromwich Albion
18:00 West Ham United Vs Arsenal
20:30 Manchester City Vs Liverpool

Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

PAPA FRANCIS ATETEA WANYONGE WA VITA

Papa Francis akipungia mkono waumini Vatikani
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.
Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.
Alisema:
"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.
Wacha tuendelee kumuomba Mungu awaepushe wapendwa watu wa Syria na maafa zaidi, na kuziwezesha pande zilizohusika na vita kumaliza ghasia na kuruhusu msaada ufike kwa wale wanaouhitaji"
Papa Francis piya alitoa wito kwa mapigano kusitishwa Sudan Kusini na aliwaomba viongozi wa kimataifa kushughulikia zaidi yanayotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo alisema mara nyingi haitiwi maanani.
Akizungumza juu ya mamia ya wakimbizi kutoka Eritrea waliozama karibu na kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa mwezi Oktoba, alieleza wasiwasi wake kuhusu wale wanaohatarisha kila kitu ili kutafuta maisha bora.
Piya alizungumzia swala la ukatili majumbani, akitetea wanawake wanaopigwa.
Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

DIAMOND AMTAMBULISHA TENA WEMA, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA....!!!


sdd 
Tukio hilo lilitokea jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Nasikia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
994992_654719497904805_1370630389_n

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 26, 2013, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.Tafadhari Like page yetu click Jambo Tz

Wednesday, December 25, 2013

HILI NDILO BARAZA LA MAWAZIRI LINALOTAKIWA


Rais Kikwete. 
********
Baada ya kizaazaa cha wiki iliyopita ambapo mawaziri wanne walipoteza kazi zao kutokana na kuwajibishwa kwa vitendo vya ukatili na mauaji vilivyotokea wakati watendaji katika wizara zao walipokuwa wakiendesha ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ nchi nzima, kinachosubiriwa na wananchi hivi sasa ni Rais Jakaya Kikwete kuunda Baraza jipya la Mawaziri.
Kutokana na udhaifu mkubwa katika utendaji ambao kwa muda mrefu umeonyeshwa na mawaziri wengi katika Baraza la Mawaziri, hatudhani kama kuna mwananchi hata mmoja  anayemtarajia Rais Kikwete kujaza tu nafasi za mawaziri aliowafukuza wiki iliyopita.
Nderemo na vifijo vilivyotokana na furaha ya wananchi katika kila kona ya nchi baada ya mawaziri hao kuondolewa katika nyadhifa zao ni ishara tosha kwamba hawamtarajii Rais Kikwete kuishia hapo, isipokuwa kuwaondoa mawaziri wengine wengi ambao tayari wamethibitika na hata kutajwa na chama chao cha CCM kuwa ni ‘mawaziri mizigo’.

KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KWA WADAU WOTE WA JAMBO TZ

Tunapenda kuwatakia kheri ya Chistmas na Mwaka mpya wapenzi wasomaji wa blog hii na page yetu ya facebook.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili  tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

HII NDIO KADI YA CHRISTMASS TOKA KWA MHE. EDWARD NGOYAI LOWASSA KWENDA KWA WATANZANIA WOTE

Tafadhari Like ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA X-MASS DESEMBA 25, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.



 

.

Tuesday, December 24, 2013

SOMA TAARIFA KUHUSU BEI MPYA ZA UMEME ZITAKAZOANZA KUTUMIKA TAREHE 1 JANUARI 2014

tanesco
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.
Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.
Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.


Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 
Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

HII HAPA TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS


Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

WANAMUZIKI WA KUNDI LA PUSSY RIOT WAACHIWA HURU

Wanamuziki wote wa kundi la muziki wa Punk la Pussy Riot la nchini Russia wameachiliwa huru kutoka gerezani chini ya sheria ya msamaha.
Nadezhda Tolokonnikova aliachiwa huru kutoka hospitali moja ya gereza lililopo Siberia, wakati mwenzake Maria Alyokhina aliachiliwa huru Jumatatu huko Nizhny Novgorod.
Wote wameuita msamaha huo kuwa ni sawa na sarakasi za serikali za kujisafisha kabla ya kufanyika kwa michezo ya olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika Russia Februari mwakani.
Wanawake hao wanamuziki walifungwa Agosti 2012 baada ya kuimba nyimbo inayokejeli katika kanisa kuu jijini Moscow.
Kitendo chao kilitafsiriwa kama kumkufuru mungu na wananchi wengi wa Russia lakini kutiwa kwao hatiani kwa kosa la utukutu ukichochewa na chuki dhidi ya dini ulishutumiwa na vikundi vya kutetea haki za binadamu, wanaharakati wanaompinga Rais Vladmir Putin na mataifa ya nje.
Watu wengi wanaotumikia vifungo wanauona msamaha huo kama jaribio la Rais Putin la kusafisha taswira yake katika nchi za magharibi na kuiboresha rekodi yake ya haki za binadamu kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki huko Sochi Februari 2014.
Siku mbili baada ya sheria hiyo ya msamaha kuanza kutumika, Rais Putin alimsamehe Mikhail Khodorkovsky, ambaye siku za nyuma alikuwa ni mtu anayeongoza kwa utajiri nchini Russia na mkosoaji binafsi wa sera za serikali, hatua ambayo pia ilitafsiriwa kama kuyaridhisha mataifa ya magharibi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...