Adnan Januzaj akishangilia baada ya kuifungia Manchester United dhidi ya West Ham
Manchester United imeendeleza wimbi la
ushindi katika mechi ya nne mfululizo, baada ya jana kuilaza West Ham
mabao 3-1 Uwanja wa Old Trafford.
Danny Welbeck alifunga bao la kwanza
nyumbani tangu Oktoba 2012 dakika ya 26 na Adnan Januzaj akafunga la
pili dakika ya 36 kabla ya Ashley Young kumaliza kazi kwa bao la dakika
ya 72 na Carlton Cole akaifungia West Ham bao la kufutia machozi dakika
ya 81.
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Cardiff Uwanja wa Anfield jana.
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendeleza makali yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 3-1 dhidi ya Cardiff jioni hii Uwanja wa Anfield.
Nyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 25 na 45, wakati bao lingine la Liverpool lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 42 wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Jordon Mutch.
Ushindi kama huo imepata Simba SC nchini Tanzania jana wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC na Mrundi Amisi Tambwe akifunga mabao mawili moja Awadh Juma.
KWA UPANDE WA LIVERPOOL

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu click neno Jambo Tz kisha like page