Sunday, December 22, 2013
ASKARI WA MAREKANI WAJERUHIWA BOR
Jeshi la Marekani linasema kuwa
wanajeshi wake wane wamejeruhiwa Sudan Kusini pale ndege yao ilipopigwa
risasi karibu na mji wa Bor, wakijaribu kuwahamisha raia wao.
Ndege kadha zililazimika kurudi Uganda.
Jeshi la serikali ya Sudan Kusini
linajaribu kuukomboa mji wa Bor, kaskazini ya mji mkuu, Juba, kutoka
wanajeshi walioasi na kujiunga na makamo wa rais wa zamani, Riek Machar
ambaye aliuteka mji huo Jumatano.
Siku hiyo pia Marekani ilipeleka wanajeshi 45 kuwalinda raia na mali ya Marekani Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa gazeti la taifa la Uganda, New Vision,ndege mbili za jeshi la Uganda pia yalinasa katika tukio hilo.
Pamekuwa na taarifa kwenye vyombo vya
habari kutoka Sudan Kusini kwamba ndege za Uganda piya zimekuwa
zikiisaidia serikali kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi walioasi -
taarifa ambazo zinakanushwa na nchi zote mbili.
Saturday, December 21, 2013
YANGA YAKUBALI KICHAPO CHA MAGOLI 3 KWA 1 KUTOKA KWA SIMBA KATIKA MCHEZO WA KUMTAFUTA NANI MTANI JEMBE
Wachezaji
wa Timu ya Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao baada
ya kukabidhiwa kwa kuifunga Timu ya Yanga Mabao 3-1 katika mchezo wa
Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
jioni ya leo.Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na
Ramadhan Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel
Okwi.Picha zote na Othman Michuzi.
HII NDIYO RIPOTI ILIYOWANG'OA MAWAZIRI WANNE...!!!
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.
TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
KUHUSU TATHMINI YA MATATIZO YALIYOTOKANA NA OPARESHENI TOKOMEZA ;
1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:-
…Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jinsi mpango ule wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na ndani yake itashughulikia kama kulikuwa na uzembe ama kuna watu wanahusika katika kuondoa maisha ya watu kwa sababu za uzembe …
1.1 Kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi
Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi ulioutoa tarehe 01 Novemba, 2013 Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ilikutana Dodoma tarehe 9 Novemba, 2013 kwa lengo la kujadili utaratibu wa kutekeleza jukumu hilo.
Katika kikao hicho Kamati iliazimia kuunda Kamati Ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117(18), ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Tole la 2013 ili iweze kushughulikia suala hilo kikamilifu.

Friday, December 20, 2013
WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Leo nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa.
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza
mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi
chote cha maisha.
Wanawake
wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata
wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie
wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali
sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura
nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao
nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa
nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika
mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo
ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
Lengo
kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na
ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya
ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli
bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZ...!!! RAIS KIKWETE KUTENGUA UTEUZI WA MAZIRI WANNE...!!!
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete
amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya
'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa mapema leo bungeni.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.
Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu.

Endelea kutembelea blog hii ya Jambo Tz kwa habari zaidi. Pia usisahau ku-like page yetu ya facebook click neno Jambo Tz
RAIS KIKWETE ASAINI MUSWADA KUPINGA NA KUONDOA KODI YA SIMU...!!!
Rais Jakaya Kikwete ametia saini hati ya dharura (Certificate of Urgency) ili Muswada wa Fedha wa Mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho ya
kuondoa tozo ya kodi kwa kadi za simu.
Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2012/13
lilipitisha kodi ya Sh1,000 kwa kila kadi ya simu, hatua ambayo
ilipingwa na wabunge wengi.
Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete alitia saini
hati hiyo juma hili.
Ingawa wasemaji wa Ikulu hawakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema jana kuwa Rais Kikwete ametia saini
hati hiyo juma hili.
“Maana yake ni kuwa, muswada huo unatakiwa urudi
bungeni haraka ili uweze kufanyiwa marekebisho hayo,” alisema Makamba.
Alisema kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo, Rais alishawaagiza wadau
wanaohusika na sekta hiyo wakae na kujadili suala la kodi hizo...
“Mazungumzo hayo bado yalikuwa yanaendelea mpaka katikati ya juma hili.”
DIAMOND PLATNUMZ AFANYA PATI YA UFUSKA..!!! NAY, CHEGE, OMMY DIMPOZ WAHUDHURIA
Diamond Platnumz akimmwagia manoti Halima Kimwana.
KUFURU ya kufunga mwaka! Dogo anayejua kuzitumia vyema fursa muhimu, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefanya yake kwa mara nyingine, safari hii amefanya pati iliyojaa ufuska.
Burudani zikitolewa na Kundi la Kibao Kata.
Msanii huyo kwa ‘kolabo’ ya swahiba wake mkuu ndani ya anga la muziki
Bongo, Omari Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ alifanya tukio hilo lililoacha
watu midomo wazi mwanzoni mwa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Business Park
uliopo Kijitonyama, Dar.Pati hiyo ilikuwa ya kumpongeza mtu wake wa karibu katika Wasafi Classic Baby (WCB), Halima Haroun ‘Halima Kimwana’.
Thursday, December 19, 2013
BASI LA HOOD LAPATA AJALI MOROGORO LAUA...!!!
Upande wa chini wa basi la Hood |
Wakazi wa eneo la Doma nje kidogo ya mji wa Morogoro wakitafakari tukio kwa huzuni |
Mtu
mmoja amekufa na wengine 27 kujeruhiwa baada ya basi la Hood Limited
lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Arusha kupata ajali eneo la Melela
Mvomero, Mkoani Morogoro. CHANZO East Africa Television (EATV)
MWEKEZAJI WA SHAMBA LA KAPUNGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA
rubani wa ndege Andreas Daffee. akipongezana na wakili wake Lweikaza |
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewaachia huru watuhumiwa watatu ambao ni
Mwekezaji wa Shamba la Kapunga(Kapunga Rice Project) lililopo Wilayani
Mbarali Mkoani Mbeya ambao walikuwa wakituhumiwa kwa mashtaka matatu
ambayo ni kula njama, kumwaga sumu na kuharibu mashamba ekari 557 ya
Wananchi.
Akisoma
hukumu Mhakamani hapo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite
alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa
yakiwakabili watuhumiwa ambao ni Waldeman Veemark ambaye ni meneja wa
shamba, Sergei Beacker ambaye ni Afisa Ugani wa kampuni pamoja na rubani
wa ndege Andreas Daffee.
Mteite
alidai kuwa mbali na upande wa mashtaka kuwa na mashahidi 155,ambapo
kati yao mashahidi zaidi ya 20 hawakuweza kufika mahakamani huku wengine
9 wakitoa ushahidi wa uongo tofauti na mashtaka yaliyopelekwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)