Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Badra Masoud akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika ili kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
MPR/PR/12
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)
linasikitika kuwajulisha wateja wake wote kwamba kutawepo na upungufu wa
umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013
kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo
kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo
ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika.
Lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.
Kutokana na Matengozo hayo Mikoa
iliyounganishwa katika gridi ya Taifaa itaathirika kwa kukosa umeme kwa
baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme.
Imetolewa na: BADRA MASOUD
MENEJA UHUSIANO