MASHABIKI WA SIMBA
Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.
Zaidi ya mashabiki waliotuma ujumbe
mfupi kupitia barua pepe na wale waliopiga simu ya mkononi ya
SALEHJEMBE, wamemtaka Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na wasaidizi wake
kufikiria na kugeuza misimamo waliyonayo.
"Kweli Kibadeni anatuangusha, ni kocha
mkongwe lakini anaonyesha hana msimamo, ninahisi anaburuzwa na watu
wengine maana anatoa uamuzi ambao unaonyesha kuna chuki. Wakongwe
warudishwe," alisema Mohammed Kassim.
Juma Mroki, Thomas Mapunda waliojitambulisha wanaishi Dar es Salaam na Songea, walisema wakongwe ndiyo tatizo la timu hiyo.
"Angalia tumeongoza hadi dakika ya 90,
lakini tumeshindwa kujilinda. Uzoefu pia ni jambo muhimu, wakongwe
wasidhalauriwe eti kwa kuwa tuna vijana."
Baadhi ya wachezaji wakongwe wa Simba ambao wameshushwa kikosi cha pili ni Henry Joseph na Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Lakini mshambuliaji mwenye kasi,
Haruna Chanongo, naye ameshushwa kikosi cha pili kwa kuwa tu alishindwa
kucheza vizuri mechi moja dhidi ya Yanga!
Mashabiki Simba, jana walifanya vurugu
baada ya timu yao kushindwa kulinda bao na Kagera wakasawazisha katika
dakika za nyongeza.
Walifanya vurugu na kuvunja viti huku
baadhi yao wakiumia baada ya askari polisi kupambana nao wakati
wakijaribu kuzuia vurugu hizo.
Simba imekuwa ikisonga kwa mwendo wa
kusuasua na kusababisha kuendelea kuporomoka na sasa iko katika nafasi
ya nne baada ya Yanga walioshika usukani jana, Azam FC na Mbeya City.
Chanzo: salehjembe