Wabunge wameanza kumpinga hadharani kuhusu suala hilo ambalo jana mjadala wake uliyateka makundi ya wabunge waliokuwa wakihudhuria vikao vya kamati mbalimbali wakati wakiwa kwenye mapumziko. Katika viwanja vya Bunge jana, gazeti hili liliwashuhudia Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) na swahiba wake kisiasa, Kangi Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara (CCM) wakikataa kusaini karatasi waliyopelekewa kuunga mkono kung'olewa kwa Spika.
Baadaye kwa nyakati tofauti walisema "hoja hiyo haina mashiko" na kwamba hawakutumwa na wapigakura wao kuwania posho bungeni.
Wabunge hao walikuwa wakirejea moja ya
hoja za Dk Kigwangalla kwamba Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha
malipo ya Sh430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti,
tofauti na wajumbe wa kamati nyingine ambao malipo yao ni Sh180,000 kwa
siku.
Wengine wanaompinga Kigwangalla ni Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) na yule wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR - Mageuzi), ambao pia walisema hawaoni sababu za msingi za kumwondoa Makinda madarakani.