MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji
Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG),
Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa
Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa
kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima
Jumatano limejulishwa.Ndoa
inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na
gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge wa Viti Maalumu,
Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael
Christian wa miaka 26.
Ndoa
hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011,
imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na
majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.