Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, alipokuwa akiuaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu, katika
ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja, kuuaga mwili wa Marehemu.
Baadhi ya Wananchi mbali mbali wakiwa katika sehemu maalum nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu, ambapo utazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar, Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed Gharib Bilali,katika Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
---------------------
Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein, jana aliwaongoza mamia
ya waombolezaji katika maziko ya mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe
Marehemu
Balozi Issack Abraham Sepetu (71),aliyezikwa katika Kijiji cha Mbuzini,Mkoa wa Kusini Unguja jana Alasiri.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni
pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed
Gharib Bilal pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mapema mwili wa Balozi Sepetu uliagwa na
waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi
na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa shughuli ambayo
ilifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo
la Kikwajuni katika Manispaa ya Zanzibar kabla ya misa maalumu
iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph katika Mtaa wa Shangani.
Watoto wa marehemu, Amani,Mkusa, Wema na wengineo
walikuwapo katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na Balozi mstaafu, Ali
Abeid Karume, ambaye alisema marehemu ameacha pengo kubwa katika jamii
kwani alikuwa kiongozi makini na mzalendo aliyelipenda taifa lake.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali
Vuai,alimwelezea marehemu kama mwasisi wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka
wa kisiasa Zanzibar wakati juhudi hizo zilipoanza mara ya kwanza baada
ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi visiwani mwaka 1995 kupitia
kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Chifu Emeka Anyaoku.
No comments:
Post a Comment