*Dk. Slaa aibua mapya
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.
Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima.
Akizungumza na waandishi
wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya viongozi wa Chadema
wanaomwita msaliti.
Alisema kama wanataka awe msaliti, yupo tayari
kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata
kidogo.
Mwigamba, aliyejiunga na Chadema mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.
“Niliondoka pale makao makuu kwa mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.