Miongoni mwa matumizi yake makubwa ni
ujenzi wa makazi yake binafsi yaliyogharimu Euro 2.9 milioni (Dola 3.9
milioni), ukumbi wa chakula wenye mita za mraba 63 ambao ni pamoja na
mesi na bafu yenye thamani ya Euro 15,000.
Saturday, October 26, 2013
SIRI NZITO ZA OPERESHENI KIMBUNGA ZAFICHUKA
*******
Hivi karibuni Serikali ilianzisha operesheni maalumu iliyopewa
jina la ‘Operesheni Kimbunga’ kwa lengo la kuwaondoa nchini watu wote
ambao hawana uraia au haki ya kisheria kuishi nchini.
Baadhi ya mambo mazito yaliyoibuliwa na operesheni
hiyo ni kubainika kwa wahamiaji haramu ambao huja nchini kwa lengo la
kufanya ujangili. Aidha wengine huja maalumu kwa lengo la kufanya
ujambazi.
Kama hiyo haitoshi imebainika kwamba wapo ambao
wanakuja nchini kwa ajili ya kuuza silaha mbalimbali zikiwemo bastola na
bunduki za aina mbalimbali zikiwamo Smg kutoka Burundi nan chi zingine.
Wapo pia ambao huingia nchini kwa lengo la kulisha mifugo yao, na
uthibitisho wa hili ni kwamba wapo ng’ombe kadhaa na mifugo mingine
ambayo imekamatwan nchini ikiletwa kwa ajili ya kulishwa.
CHADEMA ARUSHA WAVURUGANA .... MWENYEKITI WA CHADEMA ARUSHA, SAMSON MWIGAMBA ASIMAMISHWA UONGOZI
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Ndugu Samson Mwigamba amesimamishwa nafasi ya uongozi hiyo mara moja kuanzia leo na Baraza la Uongozi la Kanda ya Kaskazini, huku taratibu zingine za kinidhamu zikiendelea kwa kufuata katiba, kanuni, maadili, miongozo na taratibu za chama.
Kikao hicho kimechukua hatua hizo mara moja baada ya Ndugu Mwigamba kukiri kwa maandishi kuwa ameandika kwa kutumia jina bandia na kutuma kwenye mitandao ya kijamii, kutoa tuhuma za uongo na kupotosha umma dhidi ya chama na viongozi, kinyume na katiba, kanuni, maadili, miongozo na taratibu za chama.
Hatua hiyo ya kukiri na kusimamishwa uongozi, ilifuatia baada ya Ndugu Mwigamba kutuhumiwa kusambaza katika mitandao tuhuma za uongo, upotoshaji na uchonganishi, ambapo kikao kilimwagiza kusalimisha kompyuta yake ili wataalam wa masuala ya IT wa CHADEMA, Kanda ya Kaskazini, waweze kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Thursday, October 24, 2013
MAMA KANUMBA "HUYU MCHUNGAJI KAIRUKI ANANITAFUTA KWA KUDAI KANUMBA YUPO HAI"
Baada
ya hivi karibuni kuibuka tena kwa yule nabii na Mchungaji George
Kaiuruki na kudai kuwa Marehemue Steven Kanumba bado yu hai, FROLA
Mtegoa - mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji nyota filamu wa Bongo
marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na tabia ya mtu anayejiita Nabii
George Kairuki kwa kutumia jina na kifo cha marehemu mwanaye kama njia
ya kujitengenezea fedha na umaarufu, mama Kanumba anasema kuwa awali
Kairuki alitumia msiba wa mwanaye katika kuongelea vitu ambavyo hata
familia haivijui isipo kuwa yeye pekee yake.
Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.
“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba
Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.
Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.
“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba
Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.
VATICAN YAMSIMAMISHA ASKOFU KWA KUPENDA RAHA
Kumekuwa na kelele za waumini nchini Ujerumani wakishinikiza askofu huyo afukuzwe kwa kukiuka taratibu.
Vatican City. Makao Makuu ya Kanisa
Katoliki Duniani (Vatican) yamemsimamisha kazi Askofu wa Jimbo la
Limburg, Ujerumani Franz-Peter Tebartz-van Elst anayekabiliwa na kashfa
ya matumizi mabaya ya fedha kwa shughuli za kifahari.
Vatican ilieleza jana kuwa uamuzi huo
umechukuliwa baada ya kuridhika kuwa Askofu van Elst amekiuka maadili
yaliyowekwa na Papa Francis kwa viongozi walioko chini yake akiwataka
waishi maisha ya uchaji, umaskini.
Hadi sasa, kumekuwa na kelele nyingi miongoni mwa waumini nchini Ujerumani wakitaka askofu huyo afukuzwe kazi.
M23 WAIVURUGA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
KUNDI la waasi wa M23, linalopambana
na Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
limetajwa kuwa chanzo cha kuisambaratisha Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC). Kauli hiyo imetolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, katika mahojiano yake na kituo
cha redio cha Clouds.
Membe amesema kinachosababisha
Tanzania itengwe na baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya ya EAC, ni hatua
yake ya kupeleka majeshi katika mji wa Goma ulio Mashariki mwa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa ajili ya kupambana na waasi
wanaoipinga Serikali ya Rais Joseph Kabila.
Amesema hatua hiyo ya Tanzania
ilizikera baadhi ya nchi wanachama wa EAC, zenye maslahi ya moja kwa
moja na kundi hilo na kusisitiza kuwa hata kama itatengwa, kamwe
haitaondoa vikosi vyake DRC na badala yake vitaendelea kupambana.
AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA JANA
Daladala
aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake
za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu
Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha
Bibi.
Taxi
ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari
polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika
eneo la tukio.
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).
MSAFARA WA RAIS KIKWETE WAKUMBWA NA BALAA LA MOTO MKALI
Moto mkubwa ukiteketeza msitu wa Sao Hill Mufindi |
Msafara wa rais Jakaya Kikwete ukiwa
umesimama kwa muda eneo la msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi
katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya kufuatia moto mkubwa kuwaka
katika msitu huo jana mchana.
Askari polisi akimamisha msafara wa
rais Kikwete kutokana na moto mkubwa kutanda eneo hilo la Changalawe
katika msitu wa Taifa wa Sao Hill umbali wa mita mbili kuelekea
barabara ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
Askari wa FFU wakishuka katika gari
lao kwenda kuangalia usalama wa rais Kikwete na kulia gari la kwanza
ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu
yakiwa yamesimama
hapa askari wakishuka kuingia katika
moshi mzito kuangalia usalama wa rais katika eneo hilo ambalo moshi
mzito ulitanda barabarani
ZIARA YA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA CHENGDU - CHINA
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakipata maelezo kuhusu kiwanda
cha kutengeneza maligafi za viwanda vya plastiki cha Hongda Chlor alkali
Chemical Base cha Chengdu nchini China akiwa katika ziara ya kikazi
Oktoba 22, 2013,. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah
Kigoda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa kampuni ya Dalian
International ya China kwenye hoteli ya Shangri-la, Chengdu akiwa ktika
ziara nchini China. Oktoba 22, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akikagua eneo la Mradi wa umwagiliaji la
Dujiangyan lililopo Chengdu nchini China akiwa kaika ziara nchini humo
Oktoba 22,2013.(Picha naOfisi yaWairi Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha wageni baada ya
kutembelea mradi wa umwagiliaji wa Dujiangyan uliopo Chengdu nchini
China akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 22, 2013. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, October 21, 2013
TUME YA WARIOBA YAOMBA MUDA ZAIDI
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeomba
kuongezewa muda wa mwezi mmoja kutokana na ugumu wa kazi ya uchambuzi wa
maoni yaliyotolewa na wananchi na asasi mbalimbali.
Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph
Warioba ilitakiwa kufanya kazi kwa miezi 18 kwa mujibu wa Sura ya 83 ya
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Maana yake ni kuwa Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 1, mwaka jana ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 1, mwaka huu.
Ikiwa maombi hayo ya Tume yatakubaliwa ina maana watatakiwa kukabidhi ripoti yake Desemba 1, mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji
Augustine Ramadhan aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa wamepeleka
serikalini maombi ya kuongezewa muda wa kufanya kazi.
Sunday, October 20, 2013
KENYATTA ARUHUSIWA KUTOHUDHURIA BAADHI YA VIKAO VYA KESI
Mahakama ya ICC jana
Ijumaa(18.10.2013)ilimruhusu kwa kiasi fulani Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake, ili kumpa
muda wa kushughulikia majukumu ya kisiasa.
Kenyatta , ambaye alichaguliwa kuwa
rais mwezi Machi mwaka huu, amekuwa akidai kwa muda mrefu sasa kuwa kesi
hiyo mjini The Hague itazuwia uwezo wake wa kuiongoza nchi.
"Mahakama hiyo kimsingi inamuondolea
Uhuru Kenyatta ulazima wa kuwapo wakati wote katika kesi dhidi yake
inayoanza Novemba 12, imesema mahakama hiyo ya ICC katika taarifa,
lakini ikasisitiza kuwa ni lazima afike kwa ajili ya ufunguzi wa kesi
hiyo.
Majaji wamesema kuwa ruhusa ya
Kenyatta inatolewa kwa misingi kwamba anaweze kutimiza majukumu
aliyonayo kama rais wa Kenya, na sio kwasababu ya kutoa hadhi kwa kazi
yake kama rais.
Atakuwapo wakati wa kutoa ushahidi
Mahakama hiyo iliyoko nchini Uholanzi
pia inasisitiza kuwa Kenyatta anapaswa kuwapo wakati pande zote
zitakapokuwa zinatoa taarifa zao za mwisho katika kesi hiyo, wakati
wahanga wanatoa ushahidi wao na pia,iwapo kutakuwa na haja wakati wa
kikao cha kutoa hukumu.
MSHAHARA WA RAIS KAA LA MOTO
Siku
chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto
Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.
Msimamo
wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na
utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na
Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.
Zitto
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani
Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi
(sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa
mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.
Akizungumza
na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi
kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria ya utumishi wa umma.
"Kuutaja
mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu.
Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?" alihoji.
Subscribe to:
Posts (Atom)