Tuesday, October 15, 2013

WAPINZANI KUTINGA IKULU LEO ... MKUTANO MUHIMU WA JK, MBOWE, MBATIA NA PROFESA LIPUMBA LEO UTOE MAJIBU HAYA

Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchni kutoka kushoto: James Mbatia (NCCR Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF).
Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani vyenye wabunge bungeni wanatarajia kukutana leo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam kuzungumzia utata wa baadhi ya masuala yaliyojitokeza katika mchakato unaoendelea wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kama wengi tunavyotegemea, mazungumzo hayo kwa vyovyote ni ya masuala nyeti ambayo yamesababisha mvutano na kuibua hisia kali miongoni mwa makundi ya kijamii, pengine kwa kutambua fika kwamba kupuuza madai ya wapinzani ingekuwa sawa na kumwaga petroli katika nyumba inayoungua, busara za rais wetu zimemfanya awaite viongozi wa kisiasa kuteta nao Ikulu.
Wakati viongozi hao, Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi na Profesa Ibrahimu Lipumba wanakutana na kiongozi wa nchi leo, pengine akiwa hajasaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipelekwa mezani kwake baada ya kupitishwa bungeni na wabunge wa CCM wiki chache zilizopita, watampa mwanga kilichowafanya waugomee bungeni, maana katika hotuba yake alisema ameambiwa hiki na kile sasa atasikia laivu kutoka kwao.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE, OKTOBA 15, 2013

DSC 0064 8df93
DSC 0065 72acc

KESI YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA KUUNGURUMA OKTOBA 30

sEYA11_4aa61.jpg
MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe.
Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. 

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.

KIKWETE: TUMESHINDA MAADUI ZETU

Picha_na_8_7b2d0.jpg
Rais Jakaya Kikwete amesema maadui wote ambao walitaka kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi wamedhibitiwa .
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui wote wanaohusika na kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria. "Kulikuwapo na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda adui," alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema katika siku za hivi karibuni, maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na mkakati wa kuvuruga amani ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola vimewadhibiti na nchi iko salama.
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani kwa sababu inajua wazi kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano utavurugika na shughuli za maendeleo zitasimama.

RAILA ODINGA AELEZA NYERERE ALIVYOMSAIDIA KUSOMA NJE

odinga_79ebe.jpg
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameeleza kuwa bila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada na Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.

Hata hivyo, Mzee Jaramongi aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah wa Ghana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.
Odinga alihitaji hati hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomo yake nchini Ujerumani baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule ya Maranda.
Katika kitabu hicho, Odinga alisema hakushangaa kunyimwa hati hiyo.

KLABU 7 ZATAWALA UBINGWA WA SOKA TANZANIA BARA

vodacom_premier_league_1497c.jpg
Na DANIEL MBEGA
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kutimua vumbi katika harakati za kutafuta bingwa katika mwaka wake wa 49 tangu harakati za kutafuta klabu bingwa zilipoanza mwaka 1965.
Mikiki mikiki yote hii isingekuwepo leo kama lisingekuwa wazo la kocha

wa Taifa Stars wa wakati huo, Milan Celebic wa Yugoslavia, alilolitoa mwaka 1964 kama njia ya kusaidia kuchagua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kutegemea michuano ya Sunlight Cup (sasa Taifa Cup).
Badala ya michuano ya Sunlight iliyohusisha klabu na timu za Majimbo, Celebic aliona kulikuwa na umuhimu wa kuwepo mashindano ya klabu pekee katika ngazi ya taifa na siyo yale ya mkoa, hasa wa Pwani (Dar es Salaam ya sasa), hivyo 'akaliuza' wazo lake kwa Chama cha Ligi ya Soka cha Dar es Salaam (DFLA) ambao walianzisha mashindano hayo mwaka 1965 yakijulikana kama Ligi ya Taifa.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TFA (TFF) uliofanyika kati ya Desemba 19-20, 1964 (Jumamosi na Jumapili) katika Ukumbi wa Arnautoglou mjini Dar es Salaam ndio uliojadili pamoja na mambo mengine, uanzishwaji wa Ligi ya Taifa. Tembelea jambotz8.blogspot.com na kenypino.blogspot.com kila siku.

Monday, October 14, 2013

HAYA NI MAMBO 11 YALIYOPINGWA NA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE

 Ni miaka kumi na nne sasa imepita tangu mzee wetu mpendwa baba wa taifa hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aiage dunia.
Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 22, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria . 
Alikuwa ni mototo wa chifu Burito Nyerere wa kabila dogo la wazanaki
Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani. 
Mwalimu bado ni taa inayong’aa gizani, umuhimu wake nazidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda licha ya kwanza amekwisha tuacha.
Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:

1. UJINGA 

Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache na ni mtanzania wa kwanza kupata nafasi yamasomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburg , Uingereza na kuhitimu mwaka 1952 akiwa ni gwiji wa uchumi na historia.
Mwalimu hakupenda ujinga na hivyo alipigana vita kali dhidi ya ujinga, na alifanikiwa kwa nafasi yake kuwaondoa ujinga watanzania wengi, wakiwemo viongozi wetu wa sasa ambao walisomeshwa ‘bure’ katika mazingira mazuri yakuridhisha kwa manufaa ya nchi yetu. Ndiyo maana Rais Kikwete Februari 3, 2007 alisema “….sisi tuliwekezwa na ni lazima tuwekeze kwenu ili miaka 30 ijayo Rais atoke miongoni mwenu….”

HIVI NDIVYO MKASA WA MWANDISHI WA ITV UFOO SARO ULIVYOKUWA

Mwandishi wa habari wa ITV, aliyejeruhiwa kwa risasi jana asubuhi, alilazimika kuvumilia majeraha ili kujiokoa yeye mwenyewe na wadogo zake watatu waliokuwa wakipigwa risasi, baada ya mama yake mzazi, Anastazia Saro (58), kuuawa.



Mauaji hayo ya kusikitisha, yalifanyika katika eneo la Mbezi Kibwerere, nyumbani kwa mama yake Ufoo ambako alikuwa akiishi na wadogo zake Ufoo ambao ni Goodluck, Innocent na Jonas.

Mtuhumiwa wa unyama huo ametajwa kuwa ni Anthery Mushi, ambaye ni baba mtoto wa Ufoo, na siku ya tukio wawili hao walitokea Mbezi Magari Saba nyumbani kwa Ufoo, kwenda kuzungumza kifamilia na mama mzazi wa mwandishi huyo.
Mushi (40) ni Mhandisi wa kitengo cha Mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan na aliwasili nchini juzi na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Ufoo Mbezi Mgari Saba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, Ufoo amejeruhiwa katika paja na tumboni, mama yake mzazi alikufa papo hapo baada ya kupigwa risasi ya kifuani na mtuhumiwa Mushi ambaye naye alijiua baada ya kujipiga risasi kichwani katika eneo la kidevuni.

 Walivyowasili nyumbani
Akizungumza na wavuti hii jana mdogo wake Ufoo, Goodluck alisema; "Walikuja wakiwa pamoja (Ufoo na Mushi) mapema alfajiri wakiwa ndani ya gari saa 12 kabla ya kuingia ndani walitusalimia kisha wakaingia sebuleni na kuanza mazungumzo na mama."

SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA KWA WALIMU

SERIKALI imesema, mwakani inatarajia kuajiri walimu wapya 27,000 wa shule za msingi na sekondari nchi nzima. Taarifa hiyo ilitolewa jijini hapa jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa (pichani) alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
 Alisema kwamba kitendo cha kuajiriwa kwa walimu hao, kitatoa fursa ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, kupata wanachama wengi na hivyo kuendelea kuboresha shughuli na maisha ya waajiriwa wao.
“Mwakani tunatarajia kuajiri walimu wapatao 27,000 nchi nzima na hii itakuwa ni fursa nzuri kwa mifuko ya jamii kwani watajiunga katika mifuko ya jamii iliyopo,” alisema Majaliwa.

ZITTO KABWE ATAJA MSHAHARA WA RAIS HADHARANI, ADAI NI ZAIDI YA MILIONI 380 KWA MWAKA


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ametaja mshahara anaolipwa Rais Jakaya Kikwete. Amesema kwamba kwa wadhifa alionao, Rais Kikwete analipwa zaidi ya Sh milioni 30 kwa mwezi.
Mbali na mshahara huo, Zitto amesema kiongozi huyo wa nchi, analipwa wastani wa zaidi ya Sh milioni 380 kwa mwaka ambazo ni marupurupu pamoja na mshahara wake.

Zitto aliutaja mshahara huo mjini hapa jana, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Kwa mujibu wa Zitto, hakuna sababu kwa mshahara wa kiongozi kufanywa siri kwa kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaolipa kodi inayolipa mishahara ya viongozi.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ametaja mshahara huo ikiwa ni wiki moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alisema analipwa zaidi ya Sh milioni 20 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi

MEMBE: HAKUNA KIONGOZI WA AFRIKA KUPELEKWA ICC

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea na waandishi wa habari mapema leo kwenye ukumbi wa mkutano wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Balozi Rajabu Gamaha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
Waandishi wa habari waliokusanyika kumsikiliza Mhe. Waziri Membe. 
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ukijumuisha Balozi Irene Kasyanju (kushoto), Mkurugenzi wa Kikengo cha Sheria, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mbelwa Kairuki (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Balozi Dora Msechu (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika.

MWALIMU NYERERE MWENYE KADI NAMBA MOJA YANGA SC AMBAYE DAIMA ATAKUMBUKWA

nyerere_na_kikwete_na_kalikumtima_0ebe4.jpg
Katikati ni Mwalimu Nyerere akiwa na Katibu wa DABA wa enzi hizo, Jackson Kalikumtima kulia na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Jakaya Kikwete kushoto, sasa rais wa Jamhiri ya Muungano Tanzania. Hii ilikuwa Aprili mwaka 1998 Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Na Mahmoud Zubeiry, Bukoba
KADI namba moja ya uanachama wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, inadaiwa alipewa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye leo anatimiza miaka 14 tangu kifo chake, Oktoba 14, mwaka 1999.
Wakati Mwalimu Nyerere anafariki dunia, mimi nilikuwa mwandishi mchanga sana- wakati huo nipo kampuni ya Habari Corporation Limited, chini ya wamiliki wake wa awali akina Jenerali Ulimwengu.
Aliyekuwa bosi wangu wakati huo, Kenny Manara, aliyekuwa Mhariri wa gazeti DIMBA alinipa kazi ya kwenda Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru ulipowekwa mwili wa marehemu kwa ajili ya kuagwa ili kuandika habari juu ya wanamichezo waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu na kuchukua maoni yao.

Hakika nilijifunza mengi sana kupitia msiba huo kwa kusikia, kuambiwa na kujionea. Miongoni mwa niliyoambiwa ni kwamba, Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa ana kadi namba moja ya Yanga SC na kadi namba mbili, alikuwa nayo hayati Abeid Amaan Karume, rais wa zamani wa Zanzibar.
Sijabahatika kuiona 'leja' ya Yanga hadi leo tangu nisikie habari hizo, kwa hivyo siwezi kusadiki, lakini kulingana na historia ya klabu ya Yanga katika harakati za ukombozi wa taifa letu, siwezi kupinga hilo.
Nashukuru Mungu nikiwa Mwandishi wa Habari, nimewahi kufanya kazi za kuandika habari katika tukio ambalo Mwalimu Nyerere alikuwepo.

AU YATAKA ICC IAHIRISHE KESI YA KENYATTA


131013212235_kenyattareuters_043c3.jpg
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia umetaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) huko The Hague icheleweshe kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa Novemba mwaka huu.
AU pia wamekubaliana azimio linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la Afrika aliyeko madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Kucheleweshwa
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai.

Sunday, October 13, 2013

UFO SARO BADO YUKO KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI MHIMBILI

IMG_0031Pichani chini baadhi ya Wafanyakazi wenzake na Ufo Saro kutoka IPP pamoja waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Ufo Saro ambaye mpaka sasa, yuko katika chumba cha upasuaji  baada ya kupigwa risasi na mchumba wake Anteri Mushi usiku wa kuamkia leo ambapo pia alimpiga mama mzazi wa Ufo Saro Anastazia Peter Saro miaka 59 aliyefariki hapohapo  na baadae kujipiga risasi mwenyewe na kufa hapohapo, Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko Mbezi Luisi 1 2Wafanyakazi hao wakibadilishana mawazo hapa na pale katika hospitali ya Muhimbili leo hii 3 4Picha Kwa Hisani ya Fullshangwe Blog

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...