MATUKIO na vitendo viovu vinaendelea kushamiri juu ya uso wa nchi! Kijana anayedaiwa kuwa muumini wa kanisa la kilokole (jina tunalo) la jijini Dar, Faraji Oti amekutwa na mazito akidaiwa kufumaniwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jesca, Ijumaa lina kisanga kamili.
MANZESE, DAR
Tukio hilo lililoongeza furaha ya Shetani, lilichukua nafasi mwanzoni mwa wiki hii majira ya 11:00 jioni huko Manzese, jijini Dar.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na wahusika hao, kisa kilianzia kwenye simu ambapo mwenye mke alidai kunasa mawasiliano ya jamaa huyo na mkewe.
Ilidaiwa kuwa ukaribu wa wawili hao ulianzia kwenye kwaya waliyokuwa wakiitumikia kisha kuzua mawasiliano tata.
OTI AONYWA
Habari zilidai, kuna wakati mume wa Jesca alimuonya Oti kukaa mbali na mkewe lakini jamaa alipuuza huku akidaiwa kutoa maneno makali na ya dharau kwa mwenye mali.