Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda
shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka
2013 siku ya Jumatano.
Washindani 20 walishiriki mashindano
hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu
wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya
shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo
limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia
kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa
kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo
ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote
waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21,
alilia na kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa
dola 2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia
yake ya kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa
dini ya kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye
televisheni kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano
hilo miaka mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence
France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano
la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa
kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment