KLABU
za APR ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya zipo katika harakarti za kumwania
aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Simba, Juma Kaseja,
imefahamika.
Habari
za uhakika ambazo Sports Lady Blog imezinyaka zinasema viongozi wa timu
hizo wameshaanza mazungumzo na Kaseja ili kumsajili kwa msimu ujao katika nchi
hizo.
Mdau
mmoja wa soka ambaye yupo karibu na uongozi wa timu hizo, alidokeza jana kwamba,
kwa nyakati viongozi wa timu hizo mbili, wamekuwa kwenye harakati za kumsaka
Kaseja, wakiamini bado ni kipa mwenye uwezo mkubwa
langoni.
Licha
ya kutemwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao, Kaseja bado kipa namba moja
wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen, raia
wa Denmark.
Habari
zaidi zinasema, klabu ya APR iliyofika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashabiki
na Kati-Kagame Cup na kufungwa na Vital’o wiki moja iliyopira nchini Sudan,
inapewa nafasi kubwa ya kumpata kipa huyo.
Hayo
yanatokea huku Kaseja akiwa kwenye kambi ya timu ya Stars inayojiandaa na mechi
ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika kwa Nyota wa Ndani –CHAN dhidi ya Uganda
itakayopigwa Julai 13, Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam.
“Ujue
baada ya Simba kutangaza kuachana na Kaseja, kuna timu nyingi hasa za nje
zimeonesha nia ya kutaka kumsajili lakini mpaka sasa ni APR na Gor Mahia ndio
wako makini zaidi na mchakato huo,” kilisema chanzo hicho.