Tuesday, July 09, 2013
"NGUVU YA UMMA" INAVYOGHARIMU UHAI WA WAMISRI...!!!
Miili ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri ikiwa imehifadhiwa
MAAFISA wa Afya Misri wamesema takriban watu 42
wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo
wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua
wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300
wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia.
Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
NDEGE YA RAIS WA SOMALIA 'YASHIKA MOTO'
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mahamud
*******
NDEGE iliyokuwa inambeba rais wa
Somalia, imelazimika kutua kwa dharura mjini Mogadishu baada ya moja ya
mabawa yake kushika moto. (HM)Rais Hassan Sheikh Mohamud, alielezea kuwa rais hakujeruhiwa lakini wazima moto walifanya kila hali kuzima moto huo.
Bwana Mohamud alichaguliwa kama rais wa Somalia mwaka jana katika mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, katika hatua za kumaliza vita vya miaka mingi.
Mwandishi wa BBC Mohamed Mwalimu, alisema kuwa magurugumu ya ndege yaliharibiwa vibaya baada ya tukio hilo.
Rais alikuwa anaelekea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, wakati ndege hiyo ilipolazimika kurejea Mogadishu.
Moja ya ripoti zilizotolewa za mwanzo kuhusu tukio hilo, ilitoka kwa akaunti ya Twitter ya kundi la al-Shabab lakini haikusema kama imeshambulia ndege hiyo.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika pamoja na wale wa Somalia, wanaounga mkono bwana Mohamud wamewaondoa wapiganaji wa al-Shabab kutoka mji mkuu Mogadishu, mwaka jana ingawa kundi hilo bado hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia.
Serikali mpya ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kutambuliwa na serikali ya Marekani na shirika la fedha duniani (IMF).
Chanzo: bbcswahili
Monday, July 08, 2013
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AWAASA WAISLAMU NCHINI
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka Waislamu wote nchini kuishi na Watanzania wenzao katika misingi ya kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana, kama Uislamu ulivyofundisha.
Dk
Shein aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid Taqwa,
uliopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, katika hotuba ilyosomwa kwa
niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk Mwinyihaji MakameKatika hotuba hiyo ya ufunguzi wa msikiti
huo, Dk Shein alisema kuwa ni wajibu kwa Waislamu kufanya kila jitihada
katika kuilinda amani na utulivu alioubariki Mwenyezi Mungu hapa
Tanzania.
Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.
MKE WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, MAMA ANNA MKAPA AMETENGWA...!!!
MAMA ANNA MKAPA.
MKUTANO
wa wake za marais uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi wazito, akiwemo Rais wa zamani wa Marekani,
George W. Bush na Mkewe, Laura, umeacha kitendawili kizito kuhusu mke wa
Rais wa zamani, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa. Imebainika kuwa katika
mkutano huo, ambao mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma alikuwa ni
mwenyeji wao, Mama Anna Mkapa hakuhudhuria, lakini pia imeonyesha wazi
kwamba hakupewa fursa kulingana na hadhi yake.
Mkutano
huo wa Kimataifa ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es
Salaam, Juni 2-3 mwaka huu, uliozungumzia nafasi ya wanawake kuinuka
kimaendeleo, ukizihusisha taasisi zinazoendeshwa na wake wa marais,
wakiwemo wale wastaafu.
HAKEEM NA FATIMA WAAGA SHINDANO LA BBA USIKU WA LEO; MWANAMZIKI WA KIBONGO ATUMBUIZA
Ikiwa
leo ni siku ya 42 ndani ya jumba la BBA,kama inavyokuwaga siku zote
kila jumapili huwa ni eviction day yaan lazma mshirik hata mmoja aage
mashindano
Mwanadada
Fatima kutoka Malawi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuaga mashindano ya BBA
kwa usiku wa leo.Mshiriki mwenzake kutoka Malawi Natasha hakuamini
kilichotea na kuanza kulia huku Fatima akimwambia Natasha "No drama, no
drama. It's not about you, chill out "kasha akaagana na wenziwe na
kutoka nje ya jumba la BBA.
Hakeem
kutokea nchini Zimbabwe nae ameyaaga mashindano usiku wa leo huku akiwa
haamini kabisa kile kilichotokea kutokana na utani aliokuwa akiwatania
wenzake kwamba wanatoka leo.Na cha zaidi amemuacha mchumba wake CLEO
katika wakat wa majonzi.
.Usiku wa leo ndania ya BBA ulipambwa na msanii mahiri kutoka TANZANIA aitwaye WAKAZI aliyeimba nyimbo zake WEEKEND na TOUCH.
HIZI NDIYO SABABU ZA MH ZITTO KABWE KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MATUMAINI
Kupitia account yake ya facebook Mh. Zitto Kabwe amepost hotuba hii akielezea kushindwa kwake kufika katika tamasha la siku ya matumaini.
POST YAKE AMEANZA KWA KUANDIKA HIVI.
Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.
TAMASHA LA MATUMAINI
Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.
Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.
Sunday, July 07, 2013
BABU CHA MIAKA 92 AFUNGA NDOA NA BINTI ALIYEMZIDI MIAKA 70...!!!
Musali Mohammed al-Mujamaie (kulia) akiwa na mkewe, Muna Mukhlif al-Juburi. |
Mkulima
mmoja nchini Irak mwenye miaka 92 amemuoa mwanamke waliyetofautiana
miaka 70 katika ndoa tatu kwa mpigo sambamba na wajukuu zake wa kiume
wawili.
Musali
Mohammed al-Mujamaie alimuoa mke mwenye umri wa miaka 22, Muna Mukhlif
al-Juburi katika sherehe iliyodumu kwa masaa manne.
Wajukuu
zake wa kiume, wenye umri wa miaka 16 na 17, nao walifunga ndoa kwenye
sherehe hiyo iliyofanyika kaskazini mwa Baghdad Alhamisi iliyopita, kwa
mujibu wa ripoti.
Mzee Mujamaie alisema kwenye
siku hiyo maalum alikuwa akisubiria kwa muda mrefu kutokana na harusi za
wajukuu zake kuwa zinaahirishwa mara kadhaa ili aweze kuunganisha na
sherehe yake.
TBS YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA YA 'OKI'.....WADAI YANA MADHARA KIAFYA.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebaini kuwa mafuta ya kula aina ya Oki na Viking yaliyoenea sokoni nchini, yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa
mujibu wa TBS, vipimo vyote vitatu vilivyotumika kuyapima kuonyesha
ubora, vimefeli na vimeonyesha mafuta hayo kuharibika kwa haraka tangu
yalipotengenezwa na mpaka leo.
Pamoja
na Oki, mafuta mengine yenye walakini ni Asma, Vikingi, Partiner na
Premier Gold ambayo huuzwa kwa dumu lenye ujazo wa lita 20 kwa bei ya
kuanzia Sh 38,000 hadi 45,000, wakati bei ya mafuta ya kula
yanayotengenezwa nchini kwa ujazo huo huuzwa kati ya Sh. 52,000 na
Sh.55,000.
Baada
ya kupimwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora TBS, Lazaro
Msasalaga, anasema ilithibitika kuwa mafuta ya Oki yanayozalishwa
Malaysia na kupakiwa Singapore hayana ubora.
Alisema
mafuta hayo yametengenezwa 2011 na kuonyesha mwisho wa kutumika ni
Oktoba mwaka huu. Msasalaga alisema walipoyachunguza wamebaini hayana
namba ya ufuatiliaji wakati suala hilo ni la muhimu kuwekwa.
Isitoshe,
wawalipoyapima kutoka kipimo kimoja kwenda kingine, majibu yake
yalishindwa na kuzidi kuonyesha mafuta hayo kuharibika kila
walipoyapima.
Alisema kuna vipimo vya maabara ukipima vinaeleza mafuta kama yanafaa kutumika lakini kipimo hicho hakikufanikiwa.NA TALK BONGO
LUCY KOMBA NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO, KISA NDIKUMANA...!!!
MWANAFUNZI na mwalimu wake katika
sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo
kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe,
Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa,
imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha
kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza
wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe
unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho
makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai
hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo
alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe
kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia
paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku
sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua
kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni
balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu
(Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya
kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo
iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo.
SERIKALI YA AFRIKA YA KUSINI YAKANA MZEE NELSON MANDELA KUWA HANA FAHAMU
SERIKALI ya Afrika Kusini imekanusha taarifa kuwa rais wa zamani wa nchi
hiyo, Nelson Mandela, hana fahamu zake tena kama inavyoelezwa katika
nyaraka za mahakama zilizowasilishwa mnamo 26.06.2013.
Zuma alisema jana mchana baada ya kumtembelea hospitalini kuwa Madiba anapewa matibabu ya hali ya juu na timu ya madaktari bingwa waliobobea katika taaluma ya utabibu, ambao wako kando ya kitanda chake hospitalini kila wakati.
Nyaraka za mahakama zilizopatikana na shirika la habari la AFP zinaonyesha madaktari wanaomtibu Mandela walisema hana fahamu na kuishauri familia wiki moja iliyopita iruhusu mashine zinazomsaidia kuishi zizimwe ili apumzike.
MFANYABIASHARA MWENYE ASILI YA KIARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA
Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma
George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara
huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa
msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa
jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa
miezi 5.
Chiposi
alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni
mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo
licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa
kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye
alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.
Saturday, July 06, 2013
HIKI NDICHO ALICHOKISEMA JOYCE KIRIA BAADA YA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA
My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"
Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.
Nimeolewa
na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa
Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na
wasio na vyama).
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"
Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.
Subscribe to:
Posts (Atom)