Kikao
cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa
kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa
Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mchakato
wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika hatua ya rasimu na watu
mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa wakitoa maoni yao.Tayari
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa chama hicho
kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na kupata nafasi ya kuichambua,
kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ilitolewa hivi karibuni na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Habari
za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete
kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na
kuyatolea uamuzi.
Hata
hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa
cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa
lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo
wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo
zitatangazwa katika siku iliyopangwa.