Habari
za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete
kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na
kuyatolea uamuzi.
Hata
hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa
cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa
lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo
wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo
zitatangazwa katika siku iliyopangwa.
Mmoja
wa watoa habari alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi uliotolewa na kamati
hiyo, utawasilishwa kwa wanachama wake kwa utaratibu uliopangwa na
kwamba wabunge wa CCM wataelezwa katika kikao chao kitakachofanyika
keshokutwa Jumamosi katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
“Sisi
wabunge tunategemea kuelezwa uamuzi wa CC katika kikao chetu cha
Jumamosi, tumeambiwa kikao hicho ni muhimu na tuhudhurie bila kukosa,”
kilieleza chanzo hicho jana jioni.
Habari
zaidi zilisema wakuu wote wa mikoa na wilaya tayari wapo mjini Dodoma
na kwamba watakutana na Waziri Mkuu katika mkutano wa kichama uliopangwa
kufanyika jana usiku.
Zinapasha
kuwa katika mkutano huo uliotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Dodoma,
MaRC na MaDc hao wataelezwa mkakati na msimamo wa chama hicho kuhusu
mchakato wa Katiba Mpya.
CHANZO MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment