SIKU
chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth
Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini
nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao
yanazidi kuibuka.
Habari
zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na
mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea.
MTOTO WA NGWEA
Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa
jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na
mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea
mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo.
Wakati
akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza
ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo.
Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na
Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumwangalia mkoani
Dodoma.
Hata hivyo, ndugu huyo aliyekuwa akimsikiliza alimtaka mama Neema kupoa, hadi familia ikae kikao.
.
FAMILIA YAKAA KWA SAA 7, YATOA UAMUZI MZITO!
“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7,
pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa
kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,”
kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo
kwa sharti la kutotajwa gazetini, mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni
kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta
uthibitisho tutampokea.”