Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
Katoliki nchini Kardinali Pengo wakiingia katika ukumbi wa mkutano
wakati wa kikao cha Mashauriano kati ya Jeshi la Polisi na viongozi wa
makanisa ya kikatoliki uliofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi)
|
Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal
Pengo amesema viongozi wa dini hawawezi kukwepa jukumu lao la
kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua hapa nchini kwa kuwa jukumu hilo
linaanzia kwao.
Pengo
alisema kuongezeka kwa uhalifu ni changamoto kwa viongozi wa dini kwa
kuwa wao ndio wenye kazi ya kujenga maadili katika jamii na polisi
kusimamia sheria na kuwachukulia hatua wale wanaokaidi
Hayo
yalisemwa wakati wa kikao cha mashauriano kati ya Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini IGP Said Mwema vongozi wa dhehebu la Romani Katoliki
uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Naye
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar Es Salaam, Mhashimu
Eusebius Nzigilwa akisoma maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho
alisema wamekubaliana kuziimarisha kamati za ulinzi na usalama katika
nyumba za ibada zilizopo hivi sasa wakati wakiendelea kupata mafunzo ya
ukamataji salama kutoka Jeshi la Polisi.
“Parokia
ambazo hazijaunda kamati za ulinzi na usalama zihakikishe zinafanya
hivyo ndani ya mwezi huu na zile ambazo zimeundwa lakini hazifanyi kazi
mziimarishe ili kwa pamoja tuwe salama katika nyumba zetu za
ibada”Alisema Askofu Nzigilwa.
Katika
mazungumzo hayo IGP Said Mwqema alisema kwamba Viongozi wa dini wana
nafasi kubwa katika jamii ya kupunguza uhalifu kwa kuwa wao wanauwezo wa
kuwabadili watu kimatendo na kifikra kwa kufanya doria ya mwili na
roho kwa pamoja hivyo wanaweza kusaidiana na Polisi katika kupunguza
uhalifu.
No comments:
Post a Comment