SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema linafanyia kazi hoja ya klabu za Yanga
na Simba kutaka kujitoa kwenye michunao ya Kombe la Kagame zikihofia
usalama wa Sudan Kusini.
Akizunguza kwa njia ya simu jana jioni, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema baada
ya kuibuka hofu hiyo, wanafanyia kazi jambo
hilo kabla ya kutoa tamko rasmi.
“Tunalifahamu vizuri jambo hilo. Tutakaa na kujadili kwa kina kabla ya kutoa tamko rasmi,” alisema Angetile.
Kauli
ya Angetile imekuja siku moja tangu Simba na Yanga zitamke kujitoa
kwenye michuano hiyo kama itafanyika Darfur zikhofia hali ya usalama.
Juzi,
kwa nyakati tofauti viongozi wa Simba na Yanga, walisema wao
wametafakari kwa kina tahadhari ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hivyo hawakwenda
Darfur.
Viongozi
hao walitamka wazi kuliacha jambo hilo mikononi mwa TFF kuamua nini
kifanyike baada ya tahadhari ya serikali kuona nini kifanyike.