Mtuhumiwa akihojiwa na polisi
MWANAMUME
aitwaye Andrew Kabula (34), mkazi wa Kimara Mwisho jijini, hivi
karibuni alinaswa gesti akiwa na mwanafunzi ‘denti’ aliyetaka kufanya
naye ngono ili ampatie kazi bandarini..
Kabula
a.k.a Afisa Feki alijitapa kwa denti huyo kwamba ni Afisa wa Mamlaka ya
Bandari jijini Dar na ana uwezo wa kumpatia kazi kama atampa rushwa ya
ngono.
Kwa
kutambua kwamba kitendo hicho ni kosa kisheria, denti huyo (jina lake
kapuni) aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu ili kumnasa afisa huyo
feki.
Waandishi
wetu waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbezi Luis jijini Dar na
kumwekea mtego jamaa huyo katika gesti aliyoichagua, iliyopo maeneo ya
Kimara jijini Dar.
Afisa huyo kila mara alikuwa akiwasiliana na denti huku akimsisitiza kutoondoka hapo kama kweli alitaka ajira.
Waandishi, askari na denti walitangulia katika gesti hiyo na afisa akataarifiwa na denti kwamba ameshafika eneo la tukio.
Yakafuata maelekezo ya kuchukua chumba kutoka kwa afisa huyo aliyedai kwamba yupo mbali kidogo.
Saa
moja usiku, afisa feki alifika katika eneo la tukio na kuingia chumbani
katika gesti hiyo (jina tunalo), huku askari na waandishi wakifuatilia
nyendo zake.
Bila
ya kushtuka kama amewekewa mtego, moja kwa moja afisa aliingia chumbani
na kumkuta denti huyo ambaye alizidi kumsisitizia lengo lake.
Denti
aliendelea kujibaraguza na kutuma taarifa kwa askari na waandishi wetu
kwamba jamaa alikuwa tayari kwa tendo ndipo timu nzima ikavamia
chumbani.
Mara
baada ya askari kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi, afisa huyo
alipekuliwa katika simu yake ya kiganjani na kukutwa na meseji kadhaa
zikionesha kwamba alikuwa akifanya mawasiliano na wasichana wengi kwa
ajili ya kuwapa kazi bandarini.
Katika
kudhihirisha kuwa ni tapeli mzoefu, siku hiyohiyo afisa huyo alikuwa
na ahadi na msichana mwingine ambaye katika simu jina lake ‘liliseviwa’
kwa jina la Mariam ili apewe rushwa ya ngono.
Inadaiwa
kwamba, tapeli huyo amekuwa akiwadhalilisha wasichana wengi kwa staili
yake hiyo ya kuwadanganya kuwapatia kazi na kisha kuwaacha bila ya
ajira.
Baada
kutiwa nguvuni na kupelekwa Kituo cha Polisi, ilibainika kwamba jamaa
si mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari bali ni deiwaka wa udereva wa
daladala zinazofanya safari zake kati ya Ubungo na Msata mkoani Pwani.
Katika
kuonesha jamaa ni mtata, alipofikishwa kituoni na baada ya kuandikisha
maelezo alisema kwamba alikuwa akihitaji selo ya peke yake kwani hataki
kuchanganyika na watu.
Credit: GPL
No comments:
Post a Comment