Friday, June 07, 2013

TFF KUTOA TAMKO KOMBE LA KAGAME

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema linafanyia kazi hoja ya klabu za Yanga na Simba kutaka kujitoa kwenye michunao ya Kombe la Kagame zikihofia usalama wa Sudan Kusini.
Akizunguza kwa njia ya simu jana jioni, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema baada
ya kuibuka hofu hiyo, wanafanyia kazi jambo
hilo kabla ya kutoa tamko rasmi.
“Tunalifahamu vizuri jambo hilo. Tutakaa na kujadili kwa kina kabla ya kutoa tamko rasmi,” alisema Angetile.
Kauli ya Angetile imekuja siku moja tangu Simba na Yanga zitamke kujitoa kwenye michuano hiyo kama itafanyika Darfur zikhofia hali ya usalama.
Juzi, kwa nyakati tofauti viongozi wa Simba na Yanga, walisema wao wametafakari kwa kina tahadhari ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hivyo hawakwenda Darfur.
Viongozi hao walitamka wazi kuliacha jambo hilo mikononi mwa TFF kuamua nini kifanyike baada ya tahadhari ya serikali kuona nini kifanyike.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako, aliisihi TFF kufuatilia halia halisi ya usalama iliyopo Darfur.
Alisema pamoja na utayari wao kucheza michuano hiyo, TFF inao wajibu wa kufuatilia mwenendo mzima kuhusu hali ya usalama.
“Klabu tupo chini ya TFF, hivyo hatuwezi kuamua kujitoa bila ya kupata baraka kutoka kwao. Ni wajibu wao kufuatilia hali halisi kwanza na kutoa tamko juu ya ushiriki wetu,” alisema Mwalusako, juzi.
Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba,   Joseph Itang’are ‘Kinesim’ alisema pamoja na hali tete ya Darfur, bado wanasikilizia uamuzi wa mwisho wa TFF.
Alisema wakiwa washiriki, wanaendelea na maandalizi ya michuano hiyo hadi pale itakapojulikana mustakabali mzima wa michuano hiyo.
“Tunaisihi TFF kulitilia maanani jambo hili
na kutoa tamko kwamba hatuwezi kujiamualia tu wakati kuna chombo cha juu yetu,” alisema.
Michuano hiyo itakayoanza Juni 18 hadi Julai 2, itajumuisha timu tatu za Tanzania ikiwemo Super Falcon ya Zanzibar.
Wakati mara ya mwisha kwa Simba kutwaa taji hilo ni mwaka 2002, Yanga ndio bingwa mtetezi wa michuanbo hiyo baada ya kutetea taji hilo Julai 28, mwaka jana.
Timu nyingine ni Ports (Djibout), Express (Uganda), Tusker  (Kenya), Al Merreikh, El Hilary na El Ahly Shandy (Sudan), APR (Rwanda), Elman (Somalia), Vitalo’o

(Burundi) na Super Falcon ya Zanzibar

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...