Saturday, June 01, 2013
Obama atumiwa barua nyingine yenye sumu hatari aina ya Ricing.
Shirika
la upelelezi la Marekani FBI limesema kuwa barua yenye sumu hatari aina
ya ricin imetumwa kwa rais Barack Obama kutoka Spokane katika jimbo la
Washington, siku ambayo barua ya sumu kama hiyo ilipotumwa kwa Jaji wa
mahakama kuu na kwa posta.
Mtu
mmoja alikamatwa wiki iliyopita huko Spokane kuhusiana na barua hiyo
iliyotumwa kwa jaji na ambayo ilizuiliwa tarehe 14 mwezi huu.
FBI
imesema barua iliyokuwa imetumwa kwa rais Obama iligunduliwa tarehe 22
na kuongeza kuwa barua nyingine kama hiyo ilikuwa imetumwa kwenye kituo
cha ndege za kijeshi kilicho karibu.
Taarifa ya FBI na ya huduma za posta imesema kuwa barua zote 4 ziliwekewa stampu tarehe 13 Mei huko Spokane.
Tatu kati ya barua hizo zimethibitishwa kuwa na sumu ya ricin na nyingine moja bado inachunguzwa.-DW.
Friday, May 31, 2013
DIAMOND AMPIGIA MAGOTI JOKATE NA KUMUOMBA MSAMAHA
MKALI
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu
uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye
ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza
kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa
sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye
tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond
alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika
Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi
Jumanne usiku kituoni hapo.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa
nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi
yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui
niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya
kuachana kwetu na ilitokea tu.
Diamond na Jokate wakicheza.
“Naamini
hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi
kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na
alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo
hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka
moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea
kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo
hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond
alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi
kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye alisema
ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa
upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli
Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu
anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu
kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny
ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na
Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona
kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu,
hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZ...!!! NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE 2013)
Matokeo ya kidato cha 6 yametangazwa. Ufaulu umeongezeka mara dufu zaidi ya wanafunzi 90% wamefaulu. Shule zilizoongoza ni
1. Marian Girls
2. Mzumbe
Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 1
Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) 2013 - Link 2
TANGAZO MUHIMU KWA UMMA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA
Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli
hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa
Mtanzania yeyotemwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip
a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA
WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE
TOVUTI HIYO.
Kwa
taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na
Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama
ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
HAWA NDIO WADADA WALIO FUNGA NDOA YA JINSIA MOJA
Mashoga hao wakifungishwa ndoa kwenye ofisi ya msajili nchini Uingereza.
Wanawake wawili raia wa Pakistan wameweka historia kama Waislamu wa kwanza wa jinsia moja kufunga ndoa nchini Uingereza.
Rehana
Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale
walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya
msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa
wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama
wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa
na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi
meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili
hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea
vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako
mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni
kusaliti Uislamu.
Na
tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai
kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza
Kabla
ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini
kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya
Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.
Thursday, May 30, 2013
Wema Afunguka na Kusema: "Sikuwahi kumsaliti Diamond na tulikuwa tunapendana sana"
Miss
Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amefunguka
kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa katika uhusiano wake wote na Diamond
hakuwahi kumsaliti.
Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na Bongo5,amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana.
“Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.
Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”
Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.
Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na Bongo5,amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana.
“Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.
Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”
Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.
HII NDIO RIPOTI YA KUTEKWA, KUUMIZWA KIBANDA
TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL - TANGA MEI 30, 2013
UTANGULIZI:
Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam kwa maelezo kuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) ILIYOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA LEO
HOTUBA
YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO
WENJE (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa
Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji
na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali kufanya
mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:
1. Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2.
Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba
za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya
nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.
3.
Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia
ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha
kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu
moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.
4.
Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa
limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo
tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.
PICHA ZA MWAKILISHI WETU KATIKA BBA ALIVYOJIACHIA BAFUNI NA DILISH.
Dillish na Nando wakioga |
Jana
(May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika
huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi
wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa
romantic na kuonesha upendo (Romantic time).
Wakati
washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando
alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na
Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.
Huenda
huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna
pazia na uruzi wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa
kitanzania.
Dillish |
Kwa
upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi
ya kushare na Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel
akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. Jana Huddah alifunguka
na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold
digger. Lakini second kadhaa baadae akafuta kauli yake na kumwambia
kuwa alikuwa anatania. Really?!
Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi kukumbwa na Eviction.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAZIDI KUZUA UTATA
Matokeo
ya kidato cha nne yanayotarajiwa kutangazwa leo, yamezidi kuzua mapya
baada ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni
iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo
likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli.
Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
“Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
“Kwa sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu kweli,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
“Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
Chanzo
chetu kilieleza kuwa, katika kikao hicho, kulikuwa na mvutano kuhusu
kanuni ipi itumike ili kuwaokoa wanafunzi hao alama zao zisishuke.
Baada
ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda tena kuyafanyia kazi
matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa asilimia zaidi ya 20 hadi
kufikia asilimia tisa.
“Kwa sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu kweli,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Ukijaribu
kuangalia, Necta wanasimamia kanuni, lakini wakati mwingine inabidi
mtu uangalie hali ilivyo, kwa sasa watu wanaangalia zaidi mwitikio wa
wananchi utakavyokuwa haya matokeo yakitangazwa badala ya kuangalia
vitu vya msingi,” kilisema chanzo hicho.
Subscribe to:
Posts (Atom)