Akizungumza
na mwandishi wetu akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu
amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa
wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.
“Jamani
mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata
sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema
Wastara.
Wastara
alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure kwa sababu kwa
sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado anasikia harufu ya
mumewe Sajuki.
“Bado
harufu ya Sajuki ipo mwilini mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto
wa mwenzao wanakosea sana, sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,”
alisema Wastara mwenye mtoto mdogo aliyezaa na Sajuki.