Matukio kama haya ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwauwa wenzao kwa kuwachoma moto yamekithiri katika jamii na ndiyo yaliyosababisha ajuza watatu kuuwawa kikatili usiku wa kuamkia leo huko Bunda, Mara |
MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto ajuza watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Pia
watu hao mbali na kuwaua kikatili vibibi hivyo kwa tuhuma kwamba
walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza
nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa
mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa,
tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira
kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua
kijana huyo hivi karibuni.