KESI ya kutorosha wanafunzi inayomkabili Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG), Jean Felix Bamana, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumatatu wiki hii ilianza kurindima katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Kilimanjaro huku upande wa walalamikaji ukiiambia korti, ‘mchungaji alitaka penzi bila kinga’.
Mchungaji huyo alitiwa mbaroni
Machi 13, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar akiwa na wanafunzi wawili, watoto wa familia moja, Artha Swai (17) na Angel Swai (19) ambao alidaiwa kuwatorosha kutoka mjini hapa.
Katika kesi ya msingi, mchungaji huyo alidaiwa kuwadanganya watoto hao kwamba alikuwa akiwafanyia mpango wa kwenda kusoma nje ya nchi lakini badala yake aliwaweka hotelini na kumtaka kimapenzi mmoja wao