Wednesday, May 22, 2013
UJIO WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA KUINEEMESHA SERIKALI...!!
Rais
wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya
nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya
Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai.
Katika
ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka
katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo
ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji
wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi
wa Kiafrika.
Rais
atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na
jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa
kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
Tuesday, May 21, 2013
GODBLESS LEMA AUMBUKA....VODACOM WADAI KWAMBA ULE UJUMBE WA VITISHO HAUKUTOKA KWA MKUU WA MKOA
BARUA TOKA VODACOM
KAMANDA
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amedai kuwa uchunguzi wa
awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo, umetumwa na mtandao wa simu wa nje ya nchi.
Kamanda
alisema katika ujumbe huo ambao Lema anadai uliandikwa na Mkuu wa Mkoa
Mulongo na kutumwa kwenye simu yake Aprili mwaka huu, uchunguzi wa
polisi umeonyesha kwamba haukutumwa kupitia kampuni moja wapo ya simu za
mikononi ya hapa nchini.
BABA YAKE DULLY SYKES ANASWA AKIVUTA BANGI....!!
Baba mzazi wa mwanamuziki wa bongo flava nchini Dully Sykes, Mzee Sykes pichani kama inavyoonekana akiwa na madawa haram ya kulevya aina ya bangi mkononi huku mbegu mbegu zikiwa zimedondoka chini.-----
Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa bongo flava nchini Dully Sykes , Mzee Sykes hivi karibuni alinaswa akichambua bangi mikononi mwake kwa ajili ya kuivuta.
Tukio hilo la aina yake lilitokea nyumbani kwa msanii aliyefahamika kwa jina la Shebo, na kushuhudiwa na mwandishii wetu ambae alifanikiwa kumpiga picha mzee huyo akiwa na bangi mkononi mwake.
Mzee huyo akiwa hana shaka yoyote alionekana akichambua bangi hiyo huku mbegu zake zikidondoka chini kama mchele ( picha ya juu)
Hata hivyo mzee huyo alishindwa kuendelea na zoezi la kuitayarisha bangi hiyo kutokana na kumtilia wasi wasi mwandishi akidhani ni afande.
Prof. Jay ajiunga CHADEMA Angalia PICHA
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Joseph Haule (Prof. Jay) amejiunga rasmi leo na chama cha CHADEMA.
KUTOKA JAMII FORUM, SIRI YA KIFO CHA KAMANDA BARLOW ZAVUJA. KAMANDA MUNA ATAJWA.....!!!
Sasa
ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza
ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana
kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika ukurasa wa Mbele
kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika gazeti
kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana)
Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la
Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri
zote. Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la
Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow.
Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.
" MATOKEO YA KIDATO CHA SITA".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA
MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.
“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.
"Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.
HII NDIO PRIVATE JET ATAKAYOKUWA AKIITUMIA MAKAMU WA RAISI WA KENYA RUTO
BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI DODOMA..... MACHANGU WA DAR WAKIMBILIA HUKO
BIASHARA ya ngono katika mji wa Dodoma imeshika kasi kubwa ambapo imebainika kuwa wateja wakubwa ni watumishi wa serikali, wanasiasa na madereva.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika biashara hiyo kuna makundi mbalimbali yanayotofautiana kwa malipo ya biashara hiyo.
Wapo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake ambao wamedai kuwa wanalazimika kufanya biashara hiyo kutokana na kubanwa na maisha, hususani katika marejesho ya mikopo wanaichukua kutoka katika taasisi mbalimbali ya kifedha.
Mmoja wa wafanyabiashara ya ngono (jina tunalo) bila kujua anaongea na nani, alieleza kuwa kwa sasa katika mji wa Dodoma kuna ushindani mkubwa wa biashara ya ngono kwani wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini hapa vimeteka soko hilo.
Alisema kutokana na ushindani huo kwa sasa kima cha chini ni sh 7,000 kwa mchepuo mmoja na sh 30,000 hadi 40,000 kwa kulala.
Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa wateja wakubwa wa ngono ni wafanyakazi wa serikali, wanasiasa (wabunge), madereva pamoja na wafanyakazi wa benki.
Monday, May 20, 2013
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ : MSIGWA APEWA DHAMANA
MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MCHUNGAJI MSIGWA HATIMAYE AMEPEWA DHAMANA SASA HIVI NA WENGINE 60 WALIOLETA VURUGU KUBWA SANA JANA MJINI IRINGA NA KUHARIBU MALI NYINGI SANA ZA WANANCHI
LOVENESS DIVA AMKEJELI TENA MH. ZITTO KABWE.....!!!
Baada ya kutangaza kumpiga chini Mh.Zitto Kabwe, Loveness Diva ameamua kumchokonoa tena kwa kumkejeli kuhusu uamuzi wake wa kugombea Urais.....
Huu ni ujumbe wake aliouweka instagram:
".Ivi kwa akili yako unadhani unastahili kweli kuwa Rais mteule wa taifa hili....??
"Usiponijibu nikaridhika, basi ntakuchukulia kama mtu mwenye upeo finyu asiyejua alitendalo.."
MWENYEKITI WA CHADEMA AACHIA NGAZI......!!!
Lushoto. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Lushoto, mkoani Tanga, kimepata pigo baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwekitui, Miraji Kassim kujiuzulu, kufuatia kile alichokielezea kuwa ni kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzie ngazi ya kijiji ambao wote ni wa CCM.
Mwenyekiti huyo ambaye alichaguliwa Aprili 27 mwaka huu katika uchaguzi mdogo, aliwashangaza wafuasi wake baada ya Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho Athumani Kibiriti, kusoma baraua ya kujiuzulu kwake katika mkutano wa hadhara.
Mkutano huo uliitishwa na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teklonojia, January Makamba.
YANGA: MRISHO NGASSA ATAMBULISHWA RASMI KUREJEA YANGA HII LEO
Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.
Mrisho Ngassa ambaye anarudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo kwa kutimkia kwa Matajiri wa Bongo, Azam FC na baade mwaka jana kuzwa Simba kwa Mkopo baada ya kutokea sintofahamu za kimaadili ndani ya Klabu yake hiyo.
Ngassa alienda kuichezea Simba msimu uliopita baada ya Klabu yake ya Azam kuchukizwa na kitendo chake cha kuibusu jezi ya Yanga wakati timu hizo zikicheza.
Ngassa anakuwa ni mchezaji wa kwanza kuatangazwa na klabu hiyo kumsajili muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.
MBUNGE MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA MCHANA
Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu
Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi
Subscribe to:
Posts (Atom)