Wednesday, May 08, 2013
KINANA AJIBU TUHUMA ZA MCHUNGAJI MSIGWA
Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema anaamini chanzo cha kuchafuliwa kwake na wapinzani ni wadhifa wake.
Akizungumza na mwandishi wetu Dodoma jana, Kinana alisema anaamini kuwa kama asingekuwa na wadhifa huo, asingesakamwa kwa tuhuma alizoziita za uzushi.
Aprili 29, mwaka huu, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alimtuhumu Kinana kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kudai kuwa meli iliyokuwa chini ya uwakala wa Kampuni Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa huko Vietnam na nyara hizo za Serikali.
“Hivi vitu havinisumbui. Hapa tatizo ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM. ‘I am a senior officer’ (Ofisa Mwandamizi) sasa katika chama changu kama ningekuwa nimekaa nyumbani nafanya biashara zangu yasingetokea haya.
“Nataka kuwaambia tu, waelewe kuwa hawawezi kunitoa katika ajenda yangu ya msingi. Hii ni sawa na mwanajeshi anayekwenda kupigana vita na adui halafu akawa na vikundi vidogo vinakushambulia kutoka kila upande kukutoa katika lengo la msingi... ni lazima mtu ukomae na ili ufanikiwe,” alisema Kinana.
KADINAL PENGO ASISITIZA TENA KUWA ALIYERUSHA BOMU SI MUISLAMU.......KIKWETE AWATAKA WATU WAENDELEE KUSALI
Kadinali Pengo
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.
MUSWADA WA KUZUIA MAANDAMANO NCHINI WAANDALIWA
Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana jioni kwamba serikali imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.
Waziri Nchimbi alisema kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....
Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo.
Huenda azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Ikumbukwe ni hapo juzi tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.
HILI NDO NENO LA P-FUNK MAJANI KWA LADY JAYDEE KUHUSU BIFU LA JIDE NA CLOUDS
Producer mwenye historia kubwa na ya kipekee katika muziki wa Bongo Fleva P-Funk Majani ameonesha kumuunga mkono Lady JayDee na kwamba anadhani ni muda sasa wengine wakafuata nyayo zake, yeye mwenyewe majani amemhakikishia Jide kuwa yuko nae “Count Me in”.
Ameongeza kuwa endapo wasanii na watayarishaji wa muziki wakiungana hakuna kitakachowazua isipokuwa Mungu.
Hizi ni Tweet za P-Funk Majani za May 4:
@JideJaydee I think its really high time others follow in ur Footsteps!! Count Me in!
HIKI NDICHO ALICHOSEMA JACKLINE WOLPER BAADA YA MAGAZETI KUANDIKA KUWA AMETUPIWA ZAGA ZAKE NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI
Baada ya story ya mwanadada Jacqueline wolper kutolewa nje pamoja na vitu vyake kuzagaa kwenye vyombo vya habari hususani magazeti, tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili tupate ukweli wa jambo hilo na kuamua kumtafuta hewani Jacqueline Wolper: Mwanzo nilikuwa nakaa ,Mbezi beach, kwenye apartment ya kama USD 1500 kwa mwezi, na nilikuwa nakaa mwenyewe, na kama unavyojua huwa nawalea wadogo zangu na muda huo walikuwa wapo chuo, Ila walipomaliza nikaona badala ya mimi kukaa mwenyewe ni bora nitafute nyumba nyingine mbili ili wakae wenyewe na mimi nikae mwenyewe. Ndo maana nikahama huko mbezi beach. Sa sijui hao wanaosema nimetolewa vitu nje wanatoa wapi hayo maneno. Labda kama walipiga picha wakati nahama na kuamua kujitengenezea stori. Unahisi ni kwanini wameandika kuwa umetolewa vitu nje? |
JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO..... WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCHI
Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi wa m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23 Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo....
Bisimwa anadai kwamba majeshi ya Tanzania yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale hali itakayosababisha jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI wapewa nafasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto....
Mbali na hayo, bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo , kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma.
Kikosi cha jeshi la SOUTH AFRICA kiko mita 20 kutoka waasi walipo kwenye mji wa MUNGI nje kidogo ya GOMA.
Pia aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna makomandoo 30 wa jeshi la Ufaransa ambao wako mjini GOMA na wamefikia Linda Hotel...
BUSIMWA alidai wafaransa ndio walisimamia mauaji ya kimbari ya Rwanda ,kwa hiyo kuwepo kwao ni ishara mbaya kwa wakazi wa mashariki ya CONGO ambao wengi ni watusi
HUYU NDIO MUIGIZAJI ANGA'NGANIA WATOTO WA MICHAEL JACKSON, HUU NDO USHAHIDI ALIOTOA
MUIGIZAJI nyota kutoka nchini Uingereza, Mark Lester amesema anaendelea na taratibu za kuthibitisha kuwa watoto wa Michael Jackson ni wake.
Nyota huyo amesema anaendelea na taratibu za kupima vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kwamba Prince, Prince II, na Paris pia ni watoto wake.Hayo yalibainishwa katika gazeti la Mirror nchini Uingereza.
“Siwezi kufanya vipimo vya vinasaba kama sijapata kibali kutoka kwa watoto pindi watakapokuwa kiumri na si muda mrefu wataamua mimi kufanya hivyo, nami nitafanya," alisema Nyota huyo.
Lester, ambaye aling'ara katika wimbo wa Oliver alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Michael Jackson kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Pia nyota huyo alisema, mwanadada Paris amefanana kwa kila kitu na binti yake, Olivia.
Tangu Lester aanze kutoa malalamiko yake hayo kwa mujibu wa Mirror, alisema familia ya Jackson imekata mawasiliano yote na yeye.
Kwa mujibu wa Mirror, Lester halizuiliwa kuwaona watoto tangu kifo cha Michael Jackson mwaka 2009.
Tuesday, May 07, 2013
SALAMA JABIR "AKINYONYWA ULIMI" NA NJEMBA HADHARANI......!!
Mambo vipi jamani....
Katika pitapita zangu nimefanikiwa kumnasa live Salama Jabir akinyonyana ndimi bila chenga na mwenzake...!!
Nashindwa kuthibitisha huyo wa pili ni nani na ni jinsia gani....nikimwangalia haraka haraka naona kama ni mwanaume na namfananisha na mdogo wake Wema Sepetu aitwaye Bill Sepetu.....
Nikijaribu kukaza macho kwa kwa makini, huyo wa pili namuona kama ni mwanamke kutokana na vazi lake.Hicho cha mabegani nakifananisha na sidiria za akina dada....!!
Yaani nimeumiza macho mpaka yanauma...Nashindwa kuyaamini macho yangu kuhusu Salama Jabir. Sikutegemea..!!
Chanzo Gumzo la Jiji
KIKOSI CHA MIZINGA WAFUNIKA DAR CHID BENZI ADUNDWA NA PINA
Mc mwenye VVU
Nash Mc
alifanya poa Usiku wa kikosi na mizinga 21
Kala Pina
FBI WAFIKA ARUSHA KUCHUNGUZA TUKIO LA KIGAIDI LA KANISA KUPIGWA BOMU
MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.
Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondokanchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.
FAHAMU KUHUSU DIAMOND PLATNUM KUBORONGA HUKO LONDON...... ADAM NDITI ANAYECHEZEA CHELSEA AMBWATUKA
Mtanzania ambaye kwa sasa ni raia wa Uingereza na anayechezea klabu ya Chelsea, Adam Nditi ameiponda show ya Diamond mjini Reading nchini humo na kudai ilikuwa ni aibu tupu.
“Diamond jana manyago aibu tupu waswahili lazima tubadilike it’s embarrassing,” ametweet.
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”
Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.
“Hajafanya jambo lolote ila shoo ilikuwa very unprofessional kwenye tangazo walisema inaanza saa 3 usiku jamaa amefika saa 1 asubuhi.”
“Jukwaa lilikuwa ovyo kama vile watu hawajalipa kumuuona mmoja Wa wasani wanaotamba bongo nyimbo zilikuwa zinapigwa redioni alikuwa haimbi.”
Kwa sasa Diamond yupo ziarani nchini Uingereza.
Rais Jakaya Kikwete Afanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji na Kuwateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwa wakurugenzi wa majiji
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia
--
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.
Aidha amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwawakurugenzi wa majiji.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika katika halmashauri za majiji yaArusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.
Alisema wakurugenzi walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa yaTabora, Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.
Ghasia alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe, kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye halmashauri za majiji manne kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.
Aidha amewateua na kuwapandisha vyeo wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa wawili kuwawakurugenzi wa majiji.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mabadiliko ya uongozi yamefanyika katika halmashauri za majiji yaArusha, Mwanza, Dar-es- Salaam na Mbeya.
Alisema wakurugenzi walioteuliwa na kuhamishwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa yaTabora, Sipora Liana kuwa Mkurugezni wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa mji wa Njombe, Hassan Hida kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza.
Ghasia alisema wakurugenzi waliohamishwa ni wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Zungiza kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Wilson Kabwe, kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam.
KAULI YA BUNGE KUHUSU MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA
KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA YOSEFU MFANYAKAZI PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, TAREHE 5 MEI, 2013.
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.
Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)