Monday, March 18, 2013

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA ASKARI WA TRAFIKI ALIYEGONGWA NA GARI LEO DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Saidi Mwema kuomboleza kifo cha askari WP2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari leo, Jumatatu, Machi 18, 2013 saa saba mchana katika eneo la Bamaga, Dar Es Salaam.
WP 2494 Koplo Elikiza amegongwa wakati alipokuwa anamsimamisha dereva mmoja aliyejaribu kujiunga, kinyume cha taratibu, mwishoni mwa msafara rasmi wa magari ya Mheshimiwa Rais Kikwete, alipokataa kusimama baada ya kupewa amri ya kusimama na askari huyo,  na akamgonga.
Amesema Rais Kikwete: “Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Koplo Elikiza ambaye nimejulishwa kuwa aligongwa na gari leo  akiwa kazini katika eneo la Bamaga, Dar Es Salaam, wakati alipokuwa anaongoza msafara rasmi.”
“Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kuwa Koplo Elikiza amepoteza maisha yake akiwa kazini kwenye utumishi wa jeshi lake na nchi yake, na wakati taifa letu bado linaendelea kuhitaji sana nguvukazi yake. Tutaendelea kumkumbuka kwa uaminifu wake kwa Jeshi la Polisi na kwa taifa lake la Tanzania,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Kifo chake siyo tu kwamba ni pigo kwa nchi yetu, bali ni pigo kwa Jeshi la Polisi nchini na ni pigo hasa kwa familia yake ambayo bado ilikuwa inahitaji mapenzi, uangalizi na usimamizi wa mama.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nakutumia wewe IGP salamu zangu za rambirami kuomboleza kifo hiki. Aidha, kupitia kwako nawatumia makamanda na askari wote wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuondokewa na mwenzao. Vile vile, naomba kupitia kwako unifikishie salamu za pole ya moyo wangu kwa familia ya marehemu. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huuo mkubwa na naelewa machungu yao.”

“Aidha, napenda wajue kuwa naungana nao katika kumwombea marehemu, na pia kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze pema poponi roho ya Marehemu Koplo Elikiza. Amina.

UONGOZI HALALI WA SIMBA WATUMA BARUA KWA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.

HATIMAYE LWAKATARE ATINGA MAHAKAMANI


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatale akiwasalimia wafuasi wa chama hicho kwa ishara ya vidole viwili baada ya kuwasili katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Picha zote na Jackson Odoyo



Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Chadema Wilfred Lwakatale akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Polisi baada ya kutinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

AUNT EZEKIEL ATOKA NA RADIO PRESENTER

NYOTA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amemaliza shughuli ya kuandaa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Radio Presenter’, imefahamika.

Akizungumza na Saluti5 jijini Dar es Salaam, Aunt alisema kuwa, kwenye filamu hiyo iliyoko katika mtindo wa ‘Serious Comedy’, ataonekana akicheza pamoja na nguli mwenzie, Haji Salum ‘Mboto’.
“Kiukweli, hii ni kazi yangu ambayo inaweza kuwa kali kuliko zote kwa mwaka huu, kutokana na nilivyoinakshisha kwa ubunifu wa staili ya aina ya kipekee ya uigizaji,” alisema Aunt.

HARUSI YA 2FACE YAZUA MANENO, GAVANA ATOA ZAWADI YA GARI

MWIMBAJI nyota wa African pop, Tuface Innocent maarufu kama 2face Idibia na mpenzi wake wa muda mrefu, Annie Macauley wamefunga ndoa ya kimila mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua mjadala mzito baada ya kuzawadiwa gari aina ya Prado Jeep na gavana wa Jimbo la Akwa Ibom, Dk. Godswill Akpabio.
Mbali na zawadi hiyo, gavana huyo pia ameahidi kugharamia wanafamilia 20 wa Annie anayetoka katika jimbo hilo, ambao hawana uwezo wa kwenda Dubai ambako wawili hao watafunga ndoa rasmi baadae mwezi huu
Kamishina wa mawasiliano wa jimbo hilo, Aniekan Umana, alithibitisha Alhamisi wiki hii kwamba gavana Akpabio ameamua kumsaidia Annie Idibia, hivyo familia yake na marafiki wa karibu ambao ni raia wa Akwa Ibom wasioweza kumudu gharama ya safari ya Dubai watakuwa pamoja nae kwenye sherehe hizo.

Wakati watu wakihoji sababu ya gavana huyo kuingia gharama kwa ajili ya harusi hiyo, Umana alisema kwenye taarifa ya ofisi ya jimbo kuwa, wenza hao wamefanikiwa kukusanya pamoja mastaa na watu kibao maarufu, jambo ambalo ni zuri kwa uchumi wa jimbo lake.
“Harusi ya Annie na Tuface kuletwa Akwa Ibom ni jambo zuri kwa uchumi wa jimbo, na hili lisingeliweza kutokea hata kwa matangazo ya naira milioni 3,” alisema Umana akirejea jumla ya fedha zinazotarajiwa kutumika kukata tiketi kwa familia na rafiki wa Annie kutoka Dubai.

HUYU HAPA YULE MWANAUME AMBAYE ANATARAJIWA KUFANYIWA OPARESHENI ILI KUWEKEWA UUME...

 
Historia mpya inakaribia kuandikwa duniani baada ya mwanaume ambaye anajulikana kwa jina Andrew Wardle, kutoka Stalybridge, Greater Manchester huko Uingereza ambaye alizaliwa bila uume, kufanya mpango wa kutengenezewa na kuwekewa kiungo hicho kwa njia ya oparesheni.

Mwanaume huyu ambaye kwa sasa anaumri wa miaka 39, anatarajiwa kuwa mwanaume wa kwanza kabisa duniani kufanyiwa oparesheni kama hii na ajabu zaidi ni kwamba, kiungo hiki kitatengenezwa kutoka sehemu ya mkono wake.
 
Andrew Wardle Katika mahojiano yake na mtandao wa The Sun, Wardle mwenyewe anasema kuwa, hakuwahi kufikiria kutokea kwa siku ambayo anaweza kupata kiungo hiki muhimu kwa mwanaume na ambacho kinafanya kazi sawasawa, na endapo itakuwa ni ya mafanikio, ataanza kuishi kama mtu wa kawaida. Madaktari kutoka chuo kikuuu cha London tayari wameshakiri ugumu wa zoezi ili lakini wamesema kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa.
Katika hali yake aliyokuwa nayo sasa, Wardle anadai kuwa amekwishawahi kulala na zaidi ya wanawake 100, na asilimia 20% tu ya wanawake hawa ndio alioweza kuwaambia ukweli.
Wardle kwa sasa anafanya kazi kama mlinzi, mpishi na mhudumu na katika historia yake, amekwishapata matukio mbalimbali ya kunyanyaswa kutokana na hali yake na kupoteza marafiki kadhaa wa kike, na amekwishakuwa akijihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya kama kitu cha kumfariji.

ANGALIA ANGALIZO ALILOTOA JOHN MNYIKA

MUHIMU: Tahadhari kuna mtu amefungua akaunti kwa jina langu na picha ambayo si halali na tayari anafanya mawasiliano na kuandika vitu mbalimbali. Ifahamike wazi katika Facebook nina akaunti hii tu: http://www.facebook.com/john.mnyika?fref=ts na fan page: http://www.facebook.com/pages/John-Mnyika/113913842009362 na upande wa Twitter akaunti yangu ni: @jjmnyika pia; @TeamJohnMnyika na @TeamUbungo ambazo zipo chini ya Ofisi yangu! na blogu ni: www.mnyika.blogspot.com

Kwa wale ambao wanaona wanashindwa kuwa friends katika akaunti yangu kwasababu ya kufika ukomo basi nawaomba mjiunge na fan page yangu kwa kupitia link hii:http://www.facebook.com/pages/John-Mnyika/113913842009362na si akaunti nyingine!

Naomba tuchukue tahadhari kwa mawasiliano yoyote nje ya akaunti hizo tajwa.

Asanteni na naomba radhi kwa kadhia au usumbufu wowote uliotokea kwa yeyote kutokana na akaunti feki zilizofunguliwa kwa jina langu.

MKE WA MTU AFUMANIWA AKIZINI NA MDOGO WA MUME WAKE ( SHEMEJI YAKE)

Na Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akingonoka’ na shemeji yake.
  
Tukio hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka mtego bali ni Mungu tu.

Alieleza kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa ‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.


“Jumapili jioni walikuja tena kuniletea chakula ila kwa bahati nzuri Jumatatu nikapewa onyo na kuachiwa. Cha ajabu nilipofika nyumbani nilimkuta mtoto wangu wa miaka 2 analelewa na majirani.

“Nilipowauliza mke wangu yuko wapi walidai tangu Jumamosi hajaonekana kwa maelezo kwamba amekwenda kushughulikia dhamana yangu,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa aliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali hadi alipoamua kwenda nyumbani kwa mdogo wake.

“Nilipofika nilimkuta mke na mdogo wangu wakiwa pamoja kitandani. Baada ya mdogo wangu kuniona alinyanyuka na kuvaa bukta kisha akatoka nduki,” alisema Mrisho. 


Ikaelezwa kuwa, baada ya mwanaume huyo kumfumania mkewe huku majirani wakishuhudia, alimshushia kipigo kisha akampa talaka kabla ya kuamua kumrudisha kwao Tabora.

Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na kufumaniwa huko, Bahati alisema shemeji yake alimlazimisha kulala naye baada ya kutoka polisi kumpelekea chakula mumewe.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Rehema Dimoso alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.

TRAFIKI AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI ENEO LA BAMAGA


Trafiki Elikiza baada ya kugongwa na gari eneo la Bamaga muda huu

Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari 
eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.

SOURCE GLOBAL PUBLISHER

DEREVA ANUSURIKA KUCHARANGWA MAPANGA KWA KUMCHOMEKEA MWENZAKE IRINGA


 Dereva  wa daladala  ambae  jina lake  halikuweza  kupatikana mara moja akiwa ameshika panga mkononi akitoka kumkoromea dereva  mwenzake aliyetaka kumsababishia ajali kwa kumchomekea  eneo la Mshindo mjini Iringa  leo. PICHA NA MAELEZO FRANCIS GODWIN


 Hapa akitaka  kumcharanga mapanga  dereva  mwenzake  ,huku mwenyewe akinyosha  mikono  juu  kuomba  kusamehewa

Tabia ya  madereva  daladala  mjini Iringa  kuendesha  vyombo  hivyo bila kuzingatia  sheria limeendelea  kuongezeka na ajali   pia  kila kukicha

TUMEKUWA TUKILEA MTOTO MCHAWI KWA MUDA MREFU BILA KUJUA".....NIKITA WA BONGO MOVIE

 KELVIN....

STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Khalfan ‘Kelvin’ na mkewe mwigizaji, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’ wamesema mmoja wa watoto pacha waliowaasili (adopt) mwenye umri wa miaka sita, ameonesha matendo ya kichawi...
  

Akizungumza na mwandishi wetu, Kelvin alisema waliwachukua watoto hao mapacha kwa bibi yao Mtwara mwaka 2009 kwa lengo la kuwalea kutokana na mazingira magumu waliyokuwa nayo lakini walipofika Dar, mmoja alianza kuonesha vitendo tofauti vya kichawi.

“Wakati tukiendelea kuishi nao, tulimuona mmoja ana vitukovituko mara kwa mara na tuligundua kuwa mke wangu alikuwa akiumwaumwa kila alipomgombeza mtoto huyo.

“Kuna siku niliamka usiku kwenda kwenye chumba walichokuwa wakilala watoto hao, nikamkuta akiwa uchi akirukaruka kitandani na nilipomshtua alijilaza kitandani na asubuhi tulipomuuliza, alisema muda ule bibi yake alikuwa akimrudisha kutoka kuroga Tanga."

Kwa upande wake, Nikita alipomdadisi mtoto huyo kuhusu vitendo hivyo vya kichawi, alimwambia kuwa bibi yake anataka kumuua kwa sababu wanamzuia asirudi kijijini kwao Mtwara akaendelee kufanya kazi za kichawi. 

“Kwa kweli nampenda sana lakini sina budi kumrudisha nyumbani kwao, roho inaniuma kwa sababu nilimzoea,”alisema Nikita.

Mwandishi wetu alipomuuliza mtoto huyo kuhusiana na sakata hilo, alikiri kuwa ni kweli bibi yake ni mchawi na huwa anamchukua kwenda sehemu mbalimbali kuroga kwa kutumia usafiri wa ungo na ndiye anayemroga Nikita.

KAMPUNI YA SIMAMIA YASHUSHA MABANGO YA MATANGAZO YA KAMPUNI YA COCACOLA TAWI LA MBEYA KUTONANA NA KUDAIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 102

Wafanaya kazi wa kampuni ya Simamia wakishusha mabango ya matangazo ya biashara ya kampuni ya Cocacola tawi la Mbeya kazi ya kushusha mabango hayo imeanza maeneo ya kituo kiku cha mabasi yaendayo mikoani


Kampuni hiyo ya simamia ikiendelea na kazi ya kufuta maandishi ya kampuni ya cocacola kwa kutumia rangi nyeusi

Moja ya wakurugenzi wa kampuni ya simamia akiongea na mfanyakazi wa kampuni ya cocacolamwenye kitambulisho shingni akiulizia kulikoni mbona mnatoa mabango yetu? alipata jibu la halaka toka kwa mkurugenzi huyo kuwa mnadaiwa matangazo ya mabango tunayotoa

Mtumishi huyo wa kampuni ya cocacola nae akaungana na sisi katika kupiga picha utoaji wa mabango hayo ya kampuni yao 


Moja ya maafisa wa kampuni ya cocacola alipita hapo kituo kikuu cha mabasi ya kwenda mikoani na kujionea mwenyewe mabango yakitolewa cha ajabu mbeya yetu iliwasiliananae kwa simu jibu alilotupa kuwa hana habari kama mabango yao yanatolewa ilibidi tushangae maana picha ni hii wakati akipita standi hiyi ya mabasi akijionea uondoaji wa mabango yao


Mbali na hapo alienda moja kwa moja katika kampuni ya simamia lakini hakushuka kwenye gari yake akaondoka  kwa kasi mambo hayo




Kazi inaendelea ya kushusha mabango ya matangazo ya biashara ya kampuni ya cocacola mbeya


Mkurugenzi wa   Wakala wa kukusanya ushuru wa mabango ya biashara na Hoteli  Jiji la Mbeya Simamia Company Limited, Ndugu  Aloyce Mrema amesema kampuni yake inatekeleza sheria ya jiji ambayo inataka kila bango la tangazo linatakiwa kulipiwa.




Halimashauri ya jiji la Mbeya kupitia wakala wa ukusanyaji wa  ushuru wa mabango SIMAMIA imeyashusha mabango ya kampuni  ya Vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya kutokana na kudaiwa zaidi ya shilingi milioni 102.
Hata hivyo kampuni hiyo iko   hatiani kuburutwa mahakami kwa kushindwa kulipia gharama za mabango ya matangazo  yaliyowekwa maeneo mbali mbali ya Jiji hilo .
Kampuni hiyo imeshindwa kulipia gharama za kuweka matangazo hayo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2012 – 2013 ambapo deni limefikia Shilingi Milioni 102 ambazo walitakiwa kuzilipa kutokana na wingi wa mabango hayo.
Akithibitisha kudaiwa kwa kampuni hiyoMkurugenzi wa   Wakala wa kukusanya ushuru wa mabango ya biashara na Hoteli  Jiji la Mbeya Simamia Company Limited, Ndugu  Aloyce Mrema amesema kampuni yake inatekeleza sheria ya jiji ambayo inataka kila bango la tangazo linatakiwa kulipiwa.
Amesema kutokana na Kampuni ya Cocacola kushindwa kulipia mabango hayo kampuni ya Simamia imeamua kutoa mabango yote yaliyondani ya Jiji la Mbeya ambapo alisema hatua itakayofuata ni kuifikisha mahakamani kampuni hiyo kwa kushindwa kutekeleza agizo la Halmashauri ya Jiji.
Amesema kabla ya kuanza kutoa mabango hayo wameshapeleka  barua za kuwakumbusha zaidi tatu lakini bado hawakuitikia wito wa kulipa mapema gharama hizo zilizowataka hadi ifikapo Machi 18, Mwaka huu kutoa majibu au kulipia mabango hayo.
Mrema amesema utaratibu wa kampuni hiyo ni kuhakikisha kuwa kila kampuni iliyoweka bango la biashara katikati ya Jiji la Mbeya inalipa gharama kwa mujibu wa Sheria za Jiji ambapo kwa takayeshindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Aidha ametoa wito kwa makampuni makubwa kuheshimu sheria za nchi na siyo kukiuka kutokana na kuwa na fedha nyingi ambapo aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya makampuni sita makubwa ya Jiji la Mbeya yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo.
Hata hivyo ameyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na makampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom, Airtel,Zantel, Tbl na Pepsi ambayo yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo yakiwemo makampuni ya watu binafsi.
Akizungumzia hatua hiyo Ofisa wa Cocacola aliyejitambulisha kwa jina moja la Zekaria amesema hajui lolote kuhusu kuondolewa kwa mabango ya kampuni yake na wakala wa Jiji Simamia ambapo amesema atalifuatilia na kulipeleka kitengo kinachohusika kwa ajili ya kulitolea taarifa.
Hata hivyo Ofisa huyo alionekana kukwepa kutokuwa na taarifa juu ya kampuni hiyo kung’oa mabango ili hali baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walionekana wakipiga picha na kufuatilia hatua zote zilizokuwa zikifanyika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Haslmashauri ya Jiji la Mbeya Juma Iddi alipoulizwa juu ya utaratibu wa kampuni hiyo wa kutoa mabango ya biashara ya kampuni ya Cocacola amesema hajui lolote kwa sababu kampuni ya Simamia  ilishinda tenda ya kukusanya ushuru wa Hoteli na mabango ya biashara hivyo yeye hana uwezo wa kuingilia.
Na Mbeya yetu

TAARIFA YA RIDHIWANI KIKWETE KUKANUSHA YALIYOANDIKWA DHIDI YAKE KATIKA MITANDAO YA JAMII

Ndugu zangu habari za wikiendi. 

Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.

Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy lawas). 

Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.

Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. 

Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.

Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.

Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3. 

Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na  vyanzo vumbi na  ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka

Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo.

 Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote.

Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.

Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za uajenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.
Asanteni sana.

Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.

Sunday, March 17, 2013

LOWASSA, MENGI KUFANYIWA UMAFIA KAMA ABSALOM KIBANDA.

 EDWARD LOWASSA.
Reginald Mengi.

AFISA IKULU AHUSISHWA NA MKAKATI HUO, AFYA YA LWAKATARE YAZIDI KUDOROLA
 WAKATI sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare anayetuhumiwa kupanga mikakati ya uhalifu na kurekodiwa kwa video likizidi kuibua maswali, vigogo wengine wanadaiwa kuandaliwa mpango wa kurekodiwa kwenye video ili kuwachafua na kuwanyamazisha, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Vigogo hao ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Taarifa za mkakati huo zilisambazwa jana kwenye mtandao maarufu wa Jamii Forum, huku ukihusisha mawasilino ya ofisa mmoja wa Ikulu ya Rais Kikwete akieleza kufurahishwa kwake na kuwapongeza waliofanikisha mpango wa kuandaa video ya Lwakatare ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

AZAM FC YAMJIBU SHAFFIH DAUDA


UONGOZI WA SSB na Azam FC umesikitishwa na makala iliyotolewa na Blogu ya Shaffihdauda eti, klabu zimekuwa zikidhulumiwa na SSB na Azam FC kwa mechi zao kurushwa Live na Star TV. 

Tungependa ieleweke kuwa Azam FC ingependa kuona mashabiki wake nchini na nje ya nchi wakiiona mechi live na ndiyo maana tumekuwa tukilipia matangazo hayo, pia tunadhani hili ni jambo jema la kuungwa mkono na wadau.

Pia tungependa ifahamike kuwa kwenye kipengele cha mkataba kati ya SSB na Star TV, kuna kipengele kinachoilazimisha Star TV kutoa sehemu ya pato lake na kuvilipa vilabu ambapo kwa mechi moja klabu hupata shilingi milioni moja (1,000,000)

Kwa mechi zinazochezwa chamazi, klabu hupata mgao wa kiingilio wa chini ya shilingi laki tatu hivyo nyongeza ya milioni moja kwa mechi kurushwa live ni pesa ya kutosha angalau kwa kuanzia

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...