Monday, March 04, 2013

TAZAMA WAKENYA WANAVYOENDELEA KUPIGA KURA LEO KUMPATA MRITHI WA MWAI KIBAKI ANAYEACHIA NGAZI... MAMILIONI WAJITOKEZA... MCHUANO NI MKALI KATI YA MAWAZIRI WAKUU WA SASA UHURU KENYATTA NA ODINGA

Nachukua... nawekaa... waaaa! Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea urais, Uhuru Kenyatta akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha eneo la Gatundu nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani mkali upo baina ya Uhuru na Raila Odinga. (Picha: Reuters)
Safari hii piga ua lazima nishinde...! Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea urais kupitia Coalition for Reforms and Democracy (CORD), Raila Odinga akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha Kibera, Nairobi nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani mkali unaonekana kuwapo kati ya Odinga na Uhuru Kenyatta. (Picha: Reuters)
Odinga akijaindaa kupiga kura yake
Uhuru akiendelea na mchakato wa kumchagua mbunge wa Gatundu

SHEKH ISSA PONDA ANALO SHITAKA LA KUJIBU KATIKA KESI INAYOMKABILI


Baadhi ya wafuasi wa shekh Issa Ponda wakionyesha mikono huku wakisema takbir wakati shekh ponda akiwa katika gari la magereza mara baada ya kusomewa shitaka lake na kudai anayo kesi ya kujibu katika mahakama ya kisutu leo 


Askari magereza akimfungua pingu shekh Issa ponda katika mahakama ya kisutu  leo akisubiri kusomewa shitaka lake la kudaia kuvamia katika eneo la markazi changome bila ruhusa mwenyewe 


 Shekh Issa Ponda akisindikizwa na askari wa jeshi la magereza mara baada ya kusomewa shitaka lake leo 

WAANDISHI WA HABARI ZA UDAKU, WAMNYIMA RAHA MAMA KANUMBA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOdyu7mpsaqzAxzxVsZzLaPiSuogQ4__Sp43RUhXctlt05K51cNda3W6HI5YTlu4jnF1Ld8ryzqGNTaDCN_zROE535UYSLB1apngs8S53NkxBZb5rj907spVGWBZAke8hxonNVH_kOJIxi/s640/mama-kanumba-11.jpg

Mama yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.
mama kanumnba
Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.
“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.
Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.

WADAU WAMTUPIA MADONGO IRINE UWOYA KWA KUYAANIKA MAKALIO YAKE

Huu ni upotofu mkubwa wa maadili unaoendekezwa na hawa wanaojiita MASTAA.....

Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Uwoya ni mzazi wa mtoto mmoja ambaye walizaa na Ndikumana na hatimaya wakaachana baada ya kushindana kitabia...



Swali la kujiuliza ni kwamba, Anajisikiaje kuyaanika matako yake kwa mtoto wake wa kumzaa???...Atajenga msingi upi kwa mtoto wake akikua????.....

Achilia mbali mtoto wake, vipi juu ya wazazi wake, wadogo zake, shemeji zake na ndugu na jamaa???...
Irene jitambue.....umri umeenda sasa...unayoyafanya hayaendani na umri wako.....
Umaarufu hauji kwa kukaa uchi.....Wapo akina Lady jaydee, Monalisa....Ni wasanii maarufu pengine kuzidi hata wewe....kwa nini usiige kutoka kwao 
Kitendo hiki ni sawa na kuwatusi watazamaji wa filamu zako

UZINDUZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA TAWI LA MBEYA WAFANA


ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex Malasusa akikata utepe kuzindua chuo kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Mbeya

Viongozi mbali mbali wa mkoa wa Mbeya walihudhuria uzinduzi huo
 U
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dk. Dr.Israel Mwakyolile akisoma somo la kwanza katika ibada ya uzinduzi wa tawi hilo 
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex Malasusa Akihubiri katika ibada ya uzinduzi wa tawi la chuo kikuu cha Tumaini Makumira Uyole mbeya

WAZAZI WASHTAKIWA KWA KUMPAKA MTOTO WAO CHOCOLATE NA KUMFANANISHA NA BALOTELI

Baby 'blacked up' to look like Balotelli
HII NDIO PICHA YA MTOTO,PEMBENI NI BALOTELIWazazi wawili nchini uingereza wameshtakiwa kwa kosa la kumpaka mtoto wao Chocolate usoni na kisha kumpiga picha na kuiweka picha hiyo katika mtandao wa Twitter. Dakika chache baada ya kuiweka picha hiyo Mtandaoni watu wengi waliRT. Na haya ni baadhi ya maoni ya watu walioyatoa kuhusiana na picha hiyo



Matt Bishop, wrote: “Jesus wept, who does this to their child!?!?!?!?”
 Mwingine alisema hivi “Parents tweeted ghastly picture of baby dressed as Mario Balotelli, this must be child abuse.”  nao watetea haki za watoto hawakua nyuma, mmoja wao alitoa maoni haya “Just looking at this picture makes me very uncomfortable, especially the fact the child is blacked up. I don't like it at all.” 

MALAWI YAANZA TENA KUTISHIA NYAU WATUWAZIMA


 
Kwa ufupi
SERIKALI ya Malawi imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na kwamba hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya makubaliano ya usuluhishi.
SERIKALI ya Malawi imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na kwamba hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya makubaliano ya usuluhishi.

Kauli hiyo inakuja wakati jopo lo viongozi wastaafu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(Sadc), likijiandaa kuwasilisha ripoti yake baadaye mwezi huu.
Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, litakabidhi ripoti hiyo kwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Malawi, Ephraim Chiume, ameituhumu Tanzania kwamba imeanza kuzungumzia utatuzi wa mgogoro huo wakati ikijua kuwa mzozo huo uko katika hatua ya upatanishi maalumu.

Waziri Chiume aliikosoa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka baina ya mataifa hayo mawili, unakaribia kupatikana.
Alisema  kitendo cha  Membe kuzungumzia maendeleo ya mgogoro huo kinapingana na makubaliano ya pamoja yaliyowasilishwa kwa  Chissano na kwamba hatua hiyo inavunja moyo.

Waziri Chiume aliliambia gazeti la Nyasa Times kuwa pande zote mbili zilipokutana Nombemba 17 mwaka jana jijini Dar es Salaam, zilikubaliana kuzungumzia mgogoro huo ili kuepuka kuingilia juhudi za upatanishi. Alisema hata hivyo, hivi karibuni ya Serikali ya Tanzania imekiuka sehemu ya makubaliano hayo.
 “Tanzania wamevunja makubaliano, na sisi tunasisitiza kuwa Ziwa Nyasa ni la Malawi,” alisema waziri.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo, wamesema kauli huyo inaashiria kuwa huenda pande hizo mbili zikashindwa kukubaliana na mapandekezo yatakayowasilishwa na mpatanishi wa mzozo huo.
Mpatanishi huyo mwezi huu anatazamiwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete na yule wa Malawi, Joyce Banda.

Hata hivyo, alivyotafutwa ili kuzungumzia malalamiko hayo, waziri Membe  kupatikana, lakini Naibu wake Mahadhi Maalimu, alisema: “Ninachosema mimi kwanza hizo taarifa sijazipata na kama zipo basi Serikali itawasiliana kupitia mikondo sahihi. Serikali haiwezi kujibizana kupitia magazeti”

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania na Malawi zilipeleka barua ya pamoja kwenye Jukwaa la Marais wa Wastaafu wa Nchi za Kusini mwa Afrika linaloongozwa Chissano, zikiomba zipatanishwe katika mzozo huo.

Hatua hiyo ilikuja  baada ya majadiliano ya pande zote mbili kushindwa kuzaa matunda.
Kama sehemu ya kuepusha mgongano wa kimaslahi, jopo hilo la wasuluhishi halikuwahusisha viongozi wastaafu wa Tanzania Alhaji  Ali Hassani Mwinyi na  Benjamin Mkapa.
Hali kadhalika Bakiri Muluzi wa Malawi.

Hata hivyo, duru za kidiplomasia mjini Lilongwe zinasema  Serikali ya Malawi imejiandaa kwenda katika  Mahakama ya Haki ya Kimataifa(ICJ) kama upatanishi huo utashindwa kuzaa matunda.
Gazeti la Daily Times limewanukuu maofisa wa Serikali wakisema kuwa karata ya mwisho kwa Malawi itakuwa ni kwenda katika mahakama hiyo.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/#ixzz2Mc2j8Jzo

CCM YAMLAUMU MAALIM KWA KAULI YA "IKIBIDI LITOTE TUGAWANE MBAO"


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia lawama nzito Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  kwa kuanza kwenda kinyume na makubaliano yaliounda Serikali ya Umoaja  wa Kitaifa mwaka 2009.

Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM waliohuidhuria mkutano wa hadhara uloiofanyika Jumba la Vigae  huko Jang’ombe mjini Ungujajana(3.3.13), Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Maalim Seif ameanza kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani na umoja wa kitaifa Visiwani humu.

Vuia ambaye ni kati ya wajumbe waasisi walioshiriki katika mchakato wa mazungumzo ya upatanishi wa kisiasa Zanazibar, amesema kama angeliijua mapema dhamira ya Maalim Seif katika mazungumzo ya kundwa kwa Serikali iliyopo, angekuwa radhi kujitoa na kutokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya muafaka.
Amesema kwamba hivi karibuni kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, ameitisha kikao maalum cha vijana wa chama chake na kusema, ikiwa chama chake kitawaamrisha vijana, nchi haitatawalika na ikibidi litote tugawane mbao.

MCHAKATO WA KUCHAGUA PAPA KUANZA LEO VATICAN CITY


MAKARDINALI wa Kanisa Katoliki kutoka sehemu mbalimbali duniani, leo wanaanza maandalizi ya kumchagua mrithi wa Papa Benedict XVI, aliyeachia ngazi wiki kiliyopita.

Kwa mujibu wa tovuti ya Vatican City, ilieleza kuwa mkutano mkuu wa Makardinali utaanza leo saa 3.00 asubuhi kwa saa za Vatican (Saa 6.00 mchana kwa saa za Tanzania) kwenye Ukumbi wa New Synod Hall.

Mkutano huo ndio utafungua mchakato wa uchaguzi wa Papa mpya na unatarajiwa kuandaa ratiba ya uteuzi wa papa mpya.

Makardinali hao ndio watapanga siku ya kufanyika mkusanyiko wao unaoitwa `Papal Conclave' kwa ajili kufanya uchaguzi huo.
Papa anavyochaguliwa.

Bondia Japhet Kaseba alipomsambaratisha Maneno katika mpambano wa kuwania Ubingwa wa Taifa.


Bondia Maneno Osward kushoto akipambana na Japhert Kaseba wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa taifa uliofanyika Jumamosi katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa. Kaseba alishinda kwa point mpambano huo.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com).
Bondia Japhet Kaseba (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point.
Bondia Japhet Kaseba (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point.
Bondia Japhet Kaseba akinyooshwa mkono juu na refarii Antoni Ruta baada ya kuibuka mshindi kwa kumgalagaza Maneno Osward.
Bondia Alphonce Mchumiatumbo (kushot)o akioneshgana uwezo wa kutupiana masumbwi na Joseph Marwa mpambano wa uzito wa juu uliofanika Jumamosi. Mchumiatumbo alishinda kwa K.O raundi ya sita.
Bondia Putile Gama (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Tom Kato kutoka Japani anaeishi mjini Bagamoyo. Kato alishinda kwa K.O raundi ya pili.
Bondia Tom Kato (kulia) raia wa Japan anayeishi mjini Bagamoyo akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Putile Gama Kato alishinda kwa K.O raundi ya pili.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

WOMEN CELEBRATIONS 2013 YAFANA


 

Mama Tunu Pinda alikuwa mgeni wetu rasmi na hakuja peke yake aliongoza na wake wa viongozi wanaounda kundi la Millenium Women Group.
                                                     Mke wa waziri mkuu msaafu Mama Lowasa nae alikuwa mmoja wa wake wa viongozi waliokuwa nasi katika siku yetu #womencelebrations. walikuwa wengi kutoka Millenium Women Group wakiongozwa na mwenyekiti Mama Lukuvi. ntawaonesha wooote si mwajua raha ya 8020fashions blog ni picha...tufanye subrazinakujaaa  ::shukran kwenu Mama Zangu ,Great!!


 My Hawa alikuwa kwa Red opss GREEN carpet kukaribisha na kuongea na wageni akijua wameshona wapi na kupanda dondoo za siku yetu ta wanawake duniani. hapo alikuwa na Sabah Muchacho

Mkutano wa Hadhara na Kongamano la Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)


 
kamanda Jackson Makala akihutubia mkutano wa hadhara wa bavicha Mbulu
Kamanda Jackson Makala akizungumza wakati wa kuchangia hoja za Elimu,Rasilimali na Utawala Bora wakati wa kongamano la Vijana wa Chadema Mbulu

Sunday, March 03, 2013

CHADEMA WAENDELEZA WIMBI LA TIMUA TIMUA. HALI NI MBAYA SANA KUPITA MAELEZO


Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Morogoro kimemfukuza uanachama ndugu Dazza na kuwarudishia uanachama wao wale wote waliokuwa wamefukuzwa uanachama na Kamati Tendaji ya wilaya. Maamuzi ya kuwarudishia uanachama wao wale waliofukuzwa na Kamati Tendaji ya Wilaya ya Morogoro Mjini ulitolewa na Baraza la Uongozi la Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Susan Kiwanga Baada ya Baraza hilo kujiridhisha kuwa Kamati Tendaji ya Wilaya ilikiuka Katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama wanachama wapatao 15 pasipo kuwapa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea.

Mmoja kati ya wahanga wa maamuzi hayo ya Kamati Tendaji ya wilaya ni Mbunge Kivuri wa CHADEMA jimbo la Morogoro mjini mheshimiwa Amani Mwaipaja ambaye pia ni mwanasheria na mmiliki wa Blog ya MWAIPAJA BLOG. wito wangu kwa CHADEMA Morogoro ni kwamba wakati wa kuendekeza siasa za chuki na majungu umepitwa na wakati. Watanxzania wa leo ni waelewa kuliko wanavyofikiri CCM. Fanyeni kazi.

KENYA WAENDELEZA UBABE WAO KILIMANJARO MARATHON 2013


Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
 
Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya Dhahabu.

Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.
 
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.

TBL YATOA MSAADA WA MAGODORO 210, VYANDARUA 200 HOSPITALI MKOANI KILIMANJARO


Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), SteveKilindo (katikati), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi msaada wa magodoro kwa ajili ya Hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na Kituo cha Afya cha Uru Kiaseni katika hafla iliyofanyika Mjini Moshi. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo hicho na hospitali hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mjini Moshi . Katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimlitolewa na TBL kwa ajili ya kituo Afya cha Uru Kiaseni na Hosptali ya Uhuruma .
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL, Steve Kilindo,(katikati)wakifurahia jambo na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahm Msengi (Kulia )pamoja na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada yaTBL kukabidhi msaada wa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa kituo cha Afya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Uhuruma .
Magodoro yaliyokabidhiwa na TBL kwa Hospitali mkoani Kilimanjaro

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...