Wiki hii tumeshuhudia baadhi ya marais wastaafu wa nchi mbalimbali wakifikishwa mahakamani kusomewa mashtaka na wengine kuhukumiwa vifungo gerezani. Miongoni mwa marais hao ni:-
Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amefika mahakamani kujibu mashtaka ya ulaji wa rushwa yanayohusishwa na mkataba wa ununuzi wa silaha miaka ya tisini.
Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amefika mahakamani kujibu mashtaka ya ulaji wa rushwa yanayohusishwa na mkataba wa ununuzi wa silaha miaka ya tisini.
Baada ya Zuma (75) kufika mbele ya Mahakama Kuu kwa dakika 15 huko Durban, kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Juni.
Ameshtakiwa
kwa makosa kumi na sita ya ulaji wa rushwa, ufisadi, ulaghai na
ulanguzi wa fedha, aliyoyaepuka wakati wa utawala wake na kurejeshwa
tena mwaka 2016. Bw Zuma alitolewa madarakani kwa nguvu mwezi Februari mwaka huu.
Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geuin Hye, amehukumiwa kifungo
cha miaka 24 jela, baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi, iliyomuondoa
madarakani.
Mahakama hiyo pia imempiga faini ya takriban dola milioni 17 baada ya
kupatikana na hatia katika mashtaka kumi na sita zikiwemo, kupokea
hongo, matumizi mabaya ya madaraka na kutawala kwa vitisho.
Mahakama
iliamua kuwa Bi Park, alitumia wadhifa wake vibaya kushawishi kampuni
kuchangia fedha wakfu kadhaa zilizoongozwa na mshirika wake.
Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa zamani wa Brazil
Mahakama ya rufaa nchini Brazil Alhamisi nayo iliagiza kuwa aliyekuwa
rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, ni sharti aanze kutumikia
kifungo chake cha miaka kumi na miwili gerezani, baada ya kupatikana na
hatia ya kuhusika na ufisadi.
Majaji watano kati ya kumi na mmoja
wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watatu kati yao
wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasiwasi kisiasa nchini humo.
No comments:
Post a Comment