Viongozi kadha wa
Afrika leo wamekusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria
sherehe za kutawazwa rais mpya, Nana Akufo Addo.
Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra. Bwana
Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda
Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Madaraka yanakabidhiwa kwa kiongozi mwengine kwa salama, jambo
linaloonekana kuwa mfano mwema wa demokrasi Afrika ambako katika baadhi
ya nchi, viongozi hawataki kun'gatuka.
Baada ya kuapishwa kwa
rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya
kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani. Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
No comments:
Post a Comment