Mchezo wa mwisho wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika
kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kichapo
cha magoli 3-1 ikiwa ugenini na kuendeleza rekodi yake ya kutoshinda
michezo yake mitatu ya hatua ya nane bora msimu huu.
Bolingi alianza kuifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya 28 kipindi cha kwanza.
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent
‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu kwa
dakika zote zilizobaki.
Dakika 11 baada ya kipindi cha pili kuanza, Rainford Kalaba
aliifungia Mazembe bao la pili kabla kuongeza bao lake la pili likiwa ni
bao la tatu kwa Mazembe mnamo dakika ya 64.
Amis Tambe aliifungia Yanga bao pekee akiunganisha mpira uliogonga
‘mtambaa panya’ baada ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa adhabu ndogo.
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa pointi 13 bila kujali matokeo ya wapinzani wake Medeama na MO Bejaia.
Yanga imemaliza ikiwa nafasi ya nne (yamwisho) kwenye Kundi A ikiwa
na pointi nne baada ya kupata ushindi katika mechi moja (Yanga 1-0 MO
Bejaia) sare moja (Yanga 1-1 Medeama) huku mechi nyingine nne ikiwa
imepoteza. (MO Bejaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 TP Mazembe, Medeama 3-1
Yanga, Mazembe 3-1 Yanga).
Yanga imefunga jumla ya magoli 9 huku yenyewe ikiwa imefunga magoli manne.
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
No comments:
Post a Comment