Cristiano Ronaldo ametunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa kwa mara ya nne.
Katika msimu wa 2014/15, Ronaldo alifunga mabao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na Real Madrid. Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora.
Hii
ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya
Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.
Ronaldo,
ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, na kufika Rekodi ya mabao mengi
iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González
Blanco aliyekua kaifungia timu hiyo mabao 323. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment