Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba .
Mkazi wa Kijiji cha Saragulwa, Kata ya Nyamwilolela mkoani hapa na mwanaye wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu ambao hawajajulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati mwanamke huyo, Mageni Hongera (25) akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Joyce Ndarusanze (1), akitokea kwenye kibanda chake cha biashara kwenda nyumbani kwake.
Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba alisema jana kuwa askari wa jeshi hilo wanaendelea kufuatilia chanzo cha mauaji hayo.
“Ni kweli tukio limetokea, bado sijakusanya vizuri taarifa zake,” alisema Kakamba. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Saragulwa, Yuda Ng’hindi alisema mwanamke huyo alikatwa sehemu za shingoni na mtoto alikatwa kichwani.
Alisema mwanamke huyo alikuwa na biashara ya duka kijijini hapo na alikutwa na mkasa huo umbali wa mita kumi kabla ya kufika nyumbani kwake.
Alisema chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na kwamba uongozi wa kijiji unafuatilia kubaini wahusika wa mauaji hayo. “Tukio hilo limeacha huzuni kubwa hapa kijijini kwetu.
Alisema chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na kwamba uongozi wa kijiji unafuatilia kubaini wahusika wa mauaji hayo. “Tukio hilo limeacha huzuni kubwa hapa kijijini kwetu.
Mwanamke alikuwa anaishi vizuri na jamii. Tunaendelea kuwauliza ndugu na jamaa wa familia ile ili kujua kama kuliwahi kutokea ugomvi wowote ambao unaweza kuwa chanzo cha hayo mauaji,” alisema Ng’hindi.
Mume wa marehemu, Ndarusanze Kavula alisema majira ya saa 2:00 usiku alifika mwanaume nyumbani kwake kumpa taarifa za mkewe kupigwa na alipofuatilia alikuta ameshafariki kwa kukatwa kwa mapanga na wauaji hawajulikani.
“Alikuja raia mmoja nyumbani kwangu kunipa taarifa akipiga yowe kwamba mke wangu anapigwa huko, lakini nilipofuatilia kujua anapigwa na nani tulikuta tayari ameshafariki dunia pamoja na mwanangu.
Walikuwa na majeraha makubwa,” alisema Kavula. Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Regina Samweli (45), mkazi wa kijiji Katoro kuaawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Walikuwa na majeraha makubwa,” alisema Kavula. Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Regina Samweli (45), mkazi wa kijiji Katoro kuaawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Watu hao wanadhaniwa kuwa ni majambazi waliovamia nyumbani kwake usiku. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment