Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametetea uteuzi wa viongozi wapya ndani ya tume huku akisema wanasiasa hawatakiwi kuingilia mambo hadi jikoni.
Jaji Lubuva alisema hayo leo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Funguka kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.
"Kuhamishwa au kuteuliwa kwa kiongozi ni jambo la kawaida kwenye taasisi yoyote...uteuzi unaweza kutokea wakati wowote,"alisema Jaji Lubuva. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
"Vyama vya siasa visijiingize hadi jikoni na kuanza kulalamika.Kazi ya tume haiwezi kuathirika kwa sababu ya uteuzi uliofanywa hivi karibuni."
Mwenyekiti huyo alisisitiza kubadilishwa kwa baadhi wa watumishi wa tume isiwe chanzo kwa wanasiasa kuanza kusema NEC itashindwa kutekeza majukumu yake vizuri hasa katika kipindi hiki.
"Vyama vya siasa kujiingiza kwenye masuala yanayoihusu tume ni tatizo kwao...watu walioteuliwa wanauwezo sawa na wale waliacha nafasi hizo ndiyo maana wakachaguliwa,"alisema Jaji Lubuva.
Alisisitiza pamoja na mabadiliko hayo shughuli za NEC zitaendelea kuendeshwa kwa weledi na uadilifu.
Malalamiko hayo yamekuja baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya watendaji ndani ya tume ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa uchaguzi na mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Alipoulizwa kuhusu utoaji wa elimu ya mpigakura Jaji Lubuva alisema ikiwa kama sehemu ya majukumu ya tume, imekuwa ikifanya hivyo.
Alisema NEC inatoa elimu ya mpigakura kupitia vipindi vya televisheni,mabango na vipeperushi.
"Lakini hata vyama vya siasa pia vina jukumu la kutoa elimu kwa wapigakura,kama hili suala la wananchi kutambua Ukawa kama chama, hiyo ni nafasi nzuri kwa vyama vya siasa kutoa elimu,"alisema.
Jaji Lubuva alitumia nafasi hiyo pia kuwaonya wanasiasa waotoa kauli za kupotosha kwa wananchi kwa kuwaambia baada ya kupigakura wabaki kwenye vituo.
"Tume ilishatoa mwongozo kwamba baada ya watu kupigakura wasibaki kwenye vituo.
Mawakala wa vyama watakuwepo kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na kama wakala hataridhika na kura anahaki ya kukataa kusaini,"alisema.
Kifo cha Mchungaji Mtikila
Jaji Lubuva pia alielezea masikitiko yake kutokana na kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila aliyekufa kwa ajali ya gari na kuongeza kuwa hilo halita athiri maandalizi ya uchaguzi kwa sababu marehemu hakuwepo kwenye orodha ya wagombea waliopitishwa na tume kuwania nafasi ya urais. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment