Mtu anayedaiwa kuwa mratibu wa matukio ya ugaidi, uporaji wa silaha na mauaji katika vituo vya polisi , Ally Ulature (60) amejeruhiwa baada ya kujirusha katika ghorofa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni azimio la kujiua au kutoroka.
Akizungumza
leo, Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova
amesema Ulature ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mnandimkongo, wilayani
Mkuranga alikamatwa mwezi huu baada ya msako mkali wa polisi.
Kamanda
Kova amesema Ulature amejirusha kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la
makao makuu ya polisi alipokuwa akihojiwa na maofisa upelelezi. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
“Amejirusha
kutoka ghorofa ya tatu hadi chini baada ya kuaga kuwa anakwenda
msalani, tunadhani lengo la mtuhumiwa lilikuwa kujiua au kutoroka lakini
yote hayo hayakufanikiwa badala yake amejeruhiwa,” amesema kova
Amesema mtuhumiwa huyo amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.
Kova
amesema mtuhumiwa huyo ndiye aliyekuwa `mchoraji’ wa matukio ya uvamizi
katika vituo vya polisi vya Ikwiriri, Kimanzichana na Stakishari ambako
alisababisha mauaji na uporaji wa silaha.
Amesema
alikamatwa katika kijiji cha Mamdimkongo ambako alikuwa akiishi kwa
kujifichaficha. Kamanda Kova amewashukuru wananchi kwa ushirikiano na
kutaka waendelee ili kukomesha matukio ya uhalifu kanda ya Dar es
Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment