Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao
wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki
madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo
unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali
inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi
wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura
hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment