Maafisa
wakuu wa shirikisho la FIFA wamekubaliana kuchapisha ripoti yote kuhusu
uchunguzi wa madai ya ufisadi uliotokea wakati wa kutolewa kwa
kandarasi za kombe la dunia kwa mataifa ya Urusi mwaka 2018 na Qatar
mwaka 2022.
Wamekubaliana kutoa kurasa 430 za uchunguzi wa Michael
Garcia baada ya kufanya mkutano kufuatia pendekezo la mkuu wa kufuata
maagizo Domenica Scala.Ripoti hiyo itawekwa wazi baada ya uchunguzi unaondelea kuhusu watu watano kukamilika na inatarajiwa kufanyiwa uhariri ili kuficha majina ya mashahidi.
Hatua hiyo ya kuichapisha ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera baada ya FIFA kukataa shinikizo kutoka kwa Garcia mwenyewe na wengine kutoa ripoti hiyo.
Garcia alijiuzulu siku ya Jumatano baada ya ombi lake la kupinga ripoti fupi ya uchunguzi wake iliotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maadili katika shirikisho hilo Hans-Joachim Eckert kukataliwa.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment