Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa kauli ya serikali bungeni jana, kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji wa Wilayani Kiteto, Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda amesema Serikali itafanya mabadiliko ya kiutawala katika ngazi
mbalimbali Wilaya ya Kiteto na Mkoa wa Manyara wiki hii ili kuimarisha
uongozi kukabiliana na mauaji ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha
vifo vya watu 17 tangu Januari 12 mwaka huu hadi sasa.
Pinda alisema hayo bungeni mjini Dodoma jana
wakati akitoa taarifa kuhusu vurugu zinazoendelea Kiteto kati ya
wafugaji na wakulima na kusababisha mauaji.
Alisema mabadiliko ya uongozi wa kiutawala katika
eneo hilo ni moja ya hatua ambazo zinachukuliwa kitaifa nyingine zikiwa
ni kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya kuondoa na kuepuka na kutatua
migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Kupanga mipango ya maeneo mbalimbali wilayani
Kiteto na kutatua migogoro inayojitokeza kwa kushirikisha viongozi wa
makundi mbalimbali ya kijamii kama vile malaigwanani, wazee wa kimila na
viongozi wa dini,” alisema Pinda.
Alisema jambo lingine ni kupanga matumizi bora ya ardhi na upimaji wake katika matumizi mbalimbali na kuimilikisha kwa wananchi.
Pinda alisema hali ya mauaji Kiteto imekuwa ni ya
kujirudia, kwani Januari 12 mwaka huu, wafugaji walifanya mashambulizi
ya silaha za moto na za jadi kwa wafugaji na kusababisha vifo vya watu
10, kuteketeza pikipiki sita na mabanda 53 kuchomwa kitu ambacho
kilionyesha kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupanga.
Pinda alisema Novemba 11, mwaka huu katika Kijiji
cha Matui, mapigano ya wakulima na wafugaji yalitokea na kusababisha
vifo vya watu watano na Novemba 13 katika Kijiji cha Chekanao, wakulima
wawili waliuawa na maboma 13 kuchomwa.
“Pamoja na hali hiyo kudhibtiwa katika vijiji
hivyo, bado wananchi wana hofu juu ya maisha yao,” alisema Pinda.
Alisema Polisi Makao Makuu Dar es Salaam imetuma askari wake Mkoa wa
Manyara. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment