Mkufunzi
wa timu ya liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa anakabiliwa na tishio
la kufutwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya ya timu hiyo.
Baada
ya Liverpool kupata alama moja pekee katika mechi nne za mwisho
ilizocheza,Liverpool iko katika nafasi ya 12 katika ligi ya Uingereza
,ikiwa na alama 18 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.Miezi kadhaa iliopita ,nilikuwa mkufunzi mzuri msimu huu , na sasa mimi ninakabiliwa na tishio la kufutwa'',alisema Rodgers ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya tatu miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kushinda ligi msimu huu.
''Ni mambo ambayo makocha hukumbana nayo katika maisha ya soka'',aliongezea koch huyo.Liverpool tayari imepoteza mechi sita katika ligi msimu huu ,ikiwa ni nyingi ikilinganishwa na alama zote walizopoteza msimu uliopita.
Lakini siku ya Jumatano waliweza kupata sare ya 2-2 dhidi ya kilabu ya Ludogorets Razgad na hivyobaisi kuimarisha matumaini ya kilabu hiyo kufuzu iwapo itaichapa Fc Basel katika michuano ya muondoano ya taji la kilabu bingwa barani Ulaya.
''Kitu ambacho mtu hutakiwa kufanya ni kuendelea kujaribu kutafuta matokjeo mazuri''.,alisema Rodgers.
Kocha huyo wa zamani wa kilabu ya Swansea pia amemtetea kipa Simon Mignolet aliyeshtumiwa na mlinda lango wa zamani wa kilabu hiyo Bruce Grobbelaar. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment