Mahakama
moja nchini Misri imetupilia mbali kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa
taifa hilo Hosni Mubarak kutokana na mauaji ya mamia ya waandamanaji
wakati wa maandamano ya kumng'atua mamlakani.
Aliyekuwa waziri wa
maswala ya ndani wakati wa uongozi wa Mubarak ,Babib al Adly pamoja na
maafisa kadhaa pia wameondolewa mashtaka.Mubarak alihukumiwa miaka miwili iliopita lakini mahakama ya rufaa ikamuondela kifungo cha maisha gerezani.
Mahakama hiyo pia ilimuondolea rais huyo wa zamani mashtaka ya ufisadi.
Bwana Mubarak tayari anahudumia kifungo cha miaka mitatu kutokana na mashtaka ufujaji wa mali ya uma. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment