Ninataka kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Bin
Slum, Nassor Bin Slum nikiwa na sababu moja kubwa, BinSlum hakutaka
biashara za timu kubwa, alichoangalia ni kuzisaidia timu ndogo
zilizopanda Ligi Kuu.
Katika siku za karibuni, klabu za Mbeya City ya
Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga, zimepata
udhamini wa mamilioni na Nassor BinSlum kupitia kampuni yake ya BinSlum.
BinSlum alianza kwa kuidhamini Coastal Union ya Tanga ambayo alisema ameondoka kwenye timu hiyo kutokana na majungu.
Sitaki kuzama kwa hayo yaliyotokea Coastal Union,
lakini naipongeza kampuni hiyo inayojishughulisha na uuzaji wa betri na
matairi ya magari.
Ninataka kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Bin
Slum, Nassor Bin Slum nikiwa na sababu moja kubwa, BinSlum hakutaka
biashara za timu kubwa, alichoangalia ni kuzisaidia timu ndogo
zilizopanda Ligi Kuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Wadhamini wamekuwa na tabia ya kuangalia timu
kubwa kubwa kama Simba au Yanga. Hizi tayari ziko juu, zina rasilimali
za kutosha kujiendesha wakiwamo wanachama, lakini huku kwingine hakuna.
Mbeya City ambayo ilionyesha makali yake hata
kushika nafasi ya nne katika Ligi Kuu, inastahili kupata udhamini wa
kweli kwa kuwa wachezaji wake wameonyesha wana nia.
Hata ushiriki wao wa michuano ya Nile nchini Sudan, ilionyesha kuwa inaweza, kinachotakiwa ni kupata ‘sapoti’.
Baada ya kupata udhamini wa BinSlum, ninaamini,
Mbeya City, Ndanda FC na Stand United zitaonyesha kandanda ya ushindani
katika mechi za Ligi Kuu. Inakera kuona timu zinafungwa ovyo ovyo na
kuondoa msisimko wa ligi.
BinSlum ameingia mkataba wa miaka miwili na Mbeya
City wenye gharama ya Sh360 milioni na kila mwaka timu hiyo itakuwa
inapewa Sh180 milioni.
Stand United na Ndanda FC kila mmoja amedhaminiwa
kwa Sh50mil. Kutokana na hilo, Stand United watavaa jezi zenye logo ya
Double Star Tire sanjari na Ndanda FC.
Sasa, hapa nina mawili, kwanza nilikuwa navuta
muda kuona mdhamini mwingine anajitokeza nitoe pongezi zangu za jumla,
lakini kwa hili hapa, naamini soka itakuwa ya ushindani, kwamba timu
zilizopanda Ligi Kuu hazitatetereka sana. Pia kuna udhamini wa Azam
pamoja na Kampuni ya Vodacom.
Kingine ni kwamba, timu zilizopata udhamini zisiwaangushe walioamua kuingiza fedha zao kwao.
Hakuna mtu ambaye anaweka fedha mahali ambako hakuna hata lepe
la ushindani, na ni rahisi sana kwa mdhamini kughairi kuendelea
kuidhamini timu goigoi.
Ndiyo maana kuna wakati niliwahi kuandika hapa
kuwa timu zilizopanda Ligi Kuu ziige ilichokuwa ikifanya Mbeya City,
kwani imepanda Ligi Kuu na haikufanya mzaha hata zilipokuja timu kubwa,
Simba, Yanga, Azam haikutetereka.
Siri kubwa ni kutokuwa wanyonge na kuonyesha soka ya ushindani hata zinapokuja timu kubwa.
Hiyo itasababisha kuibuka kwa wadhamini wengine.
Mbeya City wameonyesha njia na hata wadhamini akiwamo BinSlum kujitokeza
sasa na hawa wengine iwe hivyo.
Hatutarajii kuona timu zinapata udhamini halafu
zinavurunda, haiwezekani wachezaji wakapata chao halafu wasicheze kwa
moyo, itavunja nguvu wadhamini, hilo nalisisitiza.
Ninaamini wadhamini wengine watatokea na timu
kupata fedha zitakazowapa chachu ya kuleta ushindani katika mechi zao na
isifike hatua wadhamini kusikitikia udhamini wao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment