Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo.
Utangulizi
Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya mwenendo
wa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini.Ugonjwa
huu umethibitishwabaada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu
waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es Salaam kupelekwa kwenye
maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya
homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi
ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huuni 400 na Vifo 3.
Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 ya idadi ya wagonjwa waliogundulika
mkoani Dar es salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na 4-Ilala) na
idadi ya wagonjwa waliopo wodini mpaka sasa ni 13.
Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa
mara ya
kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu 40
walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai
2013,wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
Homa ya Dengue
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.
Dengue in
ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani
asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani
matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5
hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali. Homa ya Dengue
imeshatokea katika nchi zipatazo 34 barani Afrika.
Hapa Afrika
Dengue ni ugonjwa unaojulikana kwa kiwango kidogo sana. Licha ya kwamba
milipuko ya kwanza imetokea tangu mwanzoni wa karne ya 19. Matukio ya
Ugonjwa huu yameongezeka Afrika tangu miaka ya 1980, matukio mengi
yakitokea nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na
Msumbiji, Somalia, Kenya, Komoro, Djibouti na Tanzania. Ikumbukwe kuwa
jina “Dengue” linatokana na neno “Dinga” la kiswahili linalolomaanisha
ugonjwa unaotakana na pepo yaani Kudinga pepo. Mabaharia wa Kispanish
walipokuja kwenye pwani ya Afrika Mashariki walirudi kwao na kuuita
“Dengue”.
Dalili za
ugonjwa huu ni homa, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu Dalili
hizi huanza kujitokeza kuanzia katisiku ya 3 na 14 tangu mtu
alipoambukizwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwinginedalili za
ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi
wananchi wanaombwa kuwa wakati wakipata homa kuhakikisha wanapima ili
kugundua kama wana vimelea vya malaria ua la ili hatua stahiki
zichukuliwe.
Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;
i.Homa ya dengue (Dengue Febrile Illness):
Aina hii huambatanana dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa
kichwa na maumivu ya viungo au uchovu.Aidha, kwa Tanzania mpaka sasa
zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wamejitokeza na dalili hizi.
ii.Dengue ya damu (Dengue Haemorrhagic Fever):
Aina hii yahoma ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa na
damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya
ngozi.Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza
damu nyingi kupitia kwenye michubuko.
iii.Dengue ya kupoteza fahamu (Dengue Shock syndrome):
Aina hii ya homa ya dengue huambatana na mgonjwa kupoteza damu nyingi
ambayo hupelekea mgonjwakupoteza fahamu. Dalili hizi zimeonekana kwa
mgonjwa 1 kati ya wagonjwa 400 waliokwisha kuthibitishwa kuwa na ugonjwa
hapa nchini.
Kirusi cha
homa ya Dengue kinaambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuumwa
na mbu wa Jamii ya Aedes, na hasa Aedes aegypti. Mbu huyu anaishi katika
mazingira ya makazi ya binadamu. Huuma wakati ya mchana ndani ya nyumba
au kwenye maeneo yenye vivuli, hususani majira ya asubuhi na jioni
kabla jua halijazama. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mbu huyu
anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani,
makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, vikopo, na
kadhalika. Kwa bahati mbaya mbu huyu huweza kuzaliana katika vifaa
vidogo vidogo ambavyo watu wengi huvidharau. Hivi ni pamoja na makopo ya
kuotesha maua, vikombe, vifuu vya nazi, na kadhalika. Majani mapana
yanayohifadhi maji ni mazingira mazuri kwa kuzaliana kwa mbu huyu, hivyo
maeneo ya bustani siyo ajabu kuwa mahali pazuri kwa mbu hawa.
Ugonjwa huu
hauambukizi kwa kumhudumia mgonjwa au kugusa majimaji yanayotoka kwa
mgonjwa. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa
hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka.Hakuna dawa maalumu ya
ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana nadalili
zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au
damu. Endapo mgonjwa atachelewa kupatiwa matibabu, mgonjwa anaweza
kupoteza maisha.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue
Kuangamiza mazalio ya mbu
Fukia madimbwi ya maji yaliyotuamaau nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwivya mbu kwenye madimbwi hayo
Ondoa vitu
vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi,
makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
Funika mashimo ya maji takakwa mfuniko imara
üSafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
Kujikinga na kuumwa na mbu
Tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
Hatua zinazochukuliwa na Wizara
(i)Hatua za Dharura
Uratibu
Timu ya
Taifa ya Maafa inayoshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo wa Halmashauri
za Jiji na Wadau wa Maendeleo hukutana kila mara 2 kwa wiki kutathmini
mikakati ya dharura iliyowekwa.
Uelemishaji na Uhamasishaji wa Jamii
Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa tamko la Serikali kwa nyakati tofauti
kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye
vyombo vya habari tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014.
Kuendelea
kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote
wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia
iinajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),
“Ukweli Kuhusu Ugonjwa“(Fact sheet), Mwongozo kwa watumishi wa afya wa
namna ya kuchukua sampuli. Vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga
na maambukizi ya ugonjwa huu vitatolewa.
Kuendelea
kutoa elimu kwa wananchi kupitia Radio, na Runinga. Aidha Wizara kwa
kushirikiana na Halmashauri za jiji wameendelea kutumia Maafisa
Afyaikiwemo wa kata kuwaelemisha wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa
kwakutumia vipaza sauti, uongozi wa mitaa
Mafunzo kwa watalaam wa Afya
Kuendelea
kutoa elimu ya Afya kwa Watumishi wa Afya ikiwa pamoja na madaktari na
mafundi maabara namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa
hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha kupewa
mafunzo haya na bado wanaendelea kupewa kupitia mikutano yao ya asubuhi
(Clinical meetings). Mafunzo haya pia yanaendelea kutolewa kwa vituo vya
chini kupitia Halmashauri
Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na mawasiliano
Kuimarisha
ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya
pamoja na mipakani kupitia mfumo wa saveilensi ya Wizara. Aidha, pamoja
na Mwongozo huu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa maelekezo kwa
Waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kutoa taarifa za wagonjwa
wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila juma.
Kutoa
miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu
kutokuwepo kwa aina yoyote ya vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa
wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri
anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa
watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa
Kufuatilia
kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa
Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo
kuna ugonjwa huu. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshafanya utafiti
mkoani Kagera, Morogoro na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaadhirika na
dengue.
Kuanzishwa
kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za
Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na Temeke).
Aidha, Kituo cha ‘International School of Tanganyika – IST’ kilichopo
Manispaa ya Kinondoni na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinaendelea na
ufuatiliaji wa ugonjwa huu. Aidha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
itafungua pia vituo mkoani Tanga na Mtwara, mikoa imayopakana na nchi
jirani yaani Kenya na Msumbiji ambako ugonjwa huu pia umetolewa taarifa.
·Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa Kanuni za Afya za Kimataifa uvyaoelekeza.
Upimaji na Tiba
Kuimarisha
uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa
(NHLQATC) iliyopo NIMR. Vile vile Wizara imepeleka vipimo sawia yaani
“Dengue Rapid Test Kits” kwa vituo vya Dar es Salaam kuimarisha
utambuzi. Vituo hivo ni pamoja na hospitali za Muhimbili, Amana,
Mwananyamala, Temeke Hospital, na IST kliniki. Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii imeagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha vitendanishi hivi
vinakuwepo ili kurahisisha upatikanaji wake kwa Halmashauri zote na
kupelekwa kwenye vituo vya chini zaidi. Wizara imeagiza vipimo sawia 750
vya kunyongeza ambavyo tunatarajiwa kuvipata tarehe 22.5.2014
Wizara
imeweka utaratibu wa kuhakikisha vifaa Tiba vinapatikana wakati wote
katika vituo vyote kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa watakaogundulika na
kuwa na ugonjwa huu.
Udhibiti wa mbu na mazalia
Kudhibiti
mbu kupitia kwa kupulizia na kunyunyizia viuatilifu katika baadhi ya
maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam ambayo wametoka
wagonjwa wengi wa Dengue. Hii inalenga kuangamiza mbu wapevu na
viluwiluwi.
Utafiti
Taasisi ya
Utafiti ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) iko katika maandalizi ya kufanya
utafiti kuhusu dengue kwa kuangalia maaeneo makubwa mawili.
Ukubwa wa tatizo katika binadamu
Mbu
waambukizao ugonjwa wa homa ya Dengue- kujua jamii husuka, tabia ya
kuuma watu, wapi wanapopendelea kuuma, wapi wanakozaliana kwa wingi na
mazingira yao ya kawaida.
Tafiti hizi
zinaanzia Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zote tatu (Ilala,
Kinondoni, Temeke). Tafiti zitaendelea katika baadhi ya mikoa, ikiwa ni
pamoja na mikoa 8 ambako vituo vyetu vipo.Takwimu zitakazopatikana
zitaboresha mbinu za kupambana na ugonjwa huu
(ii)Hatua za Kudumu
WAUJ imeandaa Mpango wa wa namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue. Mpango huu kwa kushirikisha sekta mbalimbali.
Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa wa Dengue
Hitimisho
Wananchi
wanashauriwa kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huu kwani hauambukizwi kwa
kumhudumia mgonjwa au kwa kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa. Hata
hivyo tunawashauri wananchi kwenda kwenye vituo vya afya haraka pindi
wanonapo dalili za ugonjwa huu.
Mlipuko wa
Dengue unadhihirisha kuwa mazingira yetu tunayoishi si salama. Ikumbukwe
kuwa, kwa sehemu kubwa, ugonjwa huu unachochewa na mazingira machafu.
Aidha mvua hizi kubwa zinazoendelea zonachangia kuongezeka kwa mazalio
ya mbu. Utupaji, uzoaji na uhifadhi wa taka katika miji yetu hauridhishi
kiasi ambacho kinatoa fursa kwa mazalio ya mbu kuongezeka na hata kuwa
karibu zaidi ya makazi ya binadamu.
Kwa kuwa,
hadi sasa hakuna chanjo wala dawa maalumu kwa ajili ya kudhibiti au
kutibu ugonjwa huu, njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu ni kumzuia
binadamu asimwe na mbu. Hivyo basi, mbinu shirikishi za kutokomeza mbu
inabidi zitiliwe mkazo katika mapambano dhidi ya homa ya Dengue. Njia
bora na rahisi ni kuhakikisha mazalio yote ya mbu yanatokomezwa. Na hili
laweza kufanywa na kila mtu kwa nafasi yake.Tunashauri watu wavae nguo
zinazofunika mikono na miguu na dawa zinazofukuza mbu (mosquito
repellent). Tunaelewa kuwa si kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua dawa
hizi na ndiyo maana tunakazania swala la kuangamiza mazalia ya mbu
ambalo ni jukumu letu wote.Tunaendelea kuhamisisha watu na hasa watoto
walale ndani ya vyandarua venye viatilifu wanapolala wakati wa mchana.
Ningependa
kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa
kuzingatia utunzaji bora wa mazingira yetu. Tukitunza mazingira yetu,
nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi yanayoambatana na mazingira
machafu.
Charles A. Pallangyo
Katibu Mkuu
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment