Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MUNGU
mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’,
amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa
hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya DengueAkifunguka
mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini
Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema
kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso
makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa
huo.
Alisema
kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia
kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari
lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu. “Huwezi
kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue,
walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa
yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima
utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika
magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu
ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana
haufai hata kidogo.
“Tena
unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama
hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.“Mateso
niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha
kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya
kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za
haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa
gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment