*Chadaiwa kuundwa na waliofukuzwa upinzani
WAKATI fukuto la kufukuzwa uanachama kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) likiwa bado bichi, chama kipya cha siasa kimeanzishwa na watu wanaodaiwa kuwa ni muungano wa wanachama waliofukuzwa kutoka vyama vya upinzani nchini.
WAKATI fukuto la kufukuzwa uanachama kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) likiwa bado bichi, chama kipya cha siasa kimeanzishwa na watu wanaodaiwa kuwa ni muungano wa wanachama waliofukuzwa kutoka vyama vya upinzani nchini.
Taarifa zilizotufikia na kuthibitishwa
na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, zinakitaja chama hicho
kuwa ni African Alliance for Change and Transparence (AACT) na kwamba
mipango ya usajili wa muda wa chama hicho inadaiwa kuanza kuratibiwa kwa
takribani mwezi mmoja sasa.
Chama hicho kimekamilisha baadhi ya
taratibu na kinatarajiwa kupewa usajili wa muda na Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa siku ya Jumanne, wiki ijayo.
Upo uwezekano wa wanachama waliofukuzwa uanachama kutoka Chadema hivi karibuni kujiunga na chama hicho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Wanasiasa wengine wanaotajwa ama kuwa
nyuma ya kuanzishwa kwa chama hicho au wanatarajia kujiunga, ni wale
waliofukuzwa kutoka CUF, nia ikiwa ni kuendeleza harakati zao za
kisiasa.
Mmoja wa watu wanaounda chama hicho
alilidokeza gazeti hili kuwa endapo chama hicho kitapata usajili baada
ya hapo, taratibu na harakati za kuanza kukitangaza zitafanyika katika
maeneo mbalimbali nchini.
Alisema pia wamepanga kuendesha siasa
zenye upinzani, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa serikali
za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 iwapo kitakuwa tayari kimejiimarisha.
Hivi karibuni Kamati Kuu Chadema,
iliwavua uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha,
Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, huku Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akikimbilia Mahakamani kuomba zuio la
kutojadiliwa uanachama wake na kikao hicho.
Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba
walituhumiwa na uongozi wa juu wa Chadema kuandaa waraka wa siri wenye
lengo la kufanya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, hali iliyoibua
mgogoro mzito hadi kufikia uamuzi wa kuwavua uanachama baadhi yao.
Alipoulizwa Dk. Kitila kama ameshiriki
na wenzake kuanzisha chama cha siasa, alishindwa kukataa wala kukubali,
kwa kusema kuwa ukweli ama uongo wa habari hiyo utajulikana.
Alipotajiwa chama hicho na kwamba kinatarajia kupata usajili wa muda, alisema hafahamu hilo na hawezi kuzungumzia.
"Sina cha kuzungumza juu ya swali
lako, kuwapo kwa chama kipya au la, nadhani ukweli utajiweka wazi nanyi
mtabaini tu, hata hilo jina la chama kipya kuitwa AACT sijui," alisema
Dk. Kitila.
Mpaka sasa vyama vya siasa vyenye
usajili wa kudumu nchini ni 23, ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, UMD,
NCCR-Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, Tadea.
Vingine ni TLP, UDP, Demokrasia
Makini, Chausta, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, Sau na AFP, UMD,
FORD, CCK, ADC na Chaumma. Chama:
Na Mtanzania
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment