Rais
wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati
akiingia kwenye uwanja wa Amani na gari la wazi kwenye maadhimisho ya
miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia
mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani
kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
Rais
wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi
waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi
vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwenye uwanja wa Amani.
Maandamano
mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za
Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa
Zanzibar na viongozi wengine.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari
wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa
wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi
cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia
silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.
Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi "Mapinduzi Daima".
Kikosi
cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar kikipita
mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed
Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja anayefahamika kwa
jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi. Picha na Adam Mzee
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed
Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka
50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo
January 12, 2014.
Vijana
wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za
miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume
leo January 12, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta
Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya
Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January
12, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri
aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya
Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea wakati
wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika
uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.PICHA NA IKULU
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment